Warning: Undefined array key 1 in /home/acaproso/public_html/._System/._Template/.Main.php on line 116
Uandishi questions

Uandishi questions | form two Kiswahili

Find Uandishi examination questions, form two Kiswahili in acaproso.com

# Question
1

Manyanda akiwa mfanyakazi wa kiwanda cha korosho Tanita alipewa taarifa kuhusu ugonjwa wa baba yake. Wewe kama Manyanda andika barua ya kuomba ruhusa. Anuani ya kiwanda ni S.L.P. 1030, Kibaha.


Short answers
2

Andika insha yenye maneno 250 kuhusu moja ya mada zifuatzo:
(a) Aisifuye mvua imemnyeshea.
(b) Elimu ya msingi ina umuhimu wake katika jamii.
(c) Maradhi yanavyorudisha nyuma maendeleo ya familia hatimaye Taifa.
(d) Kuelimika kwa msichana ni kuelimika kwa jamii.
(e) Wanyama pori.


Short answers
3

Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwako, unahitaji marafiki kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo. Andaa kadi ya mwaliko ili kuwapa taarifa rafiki zako.


Short answers
4

Wewe kama afisa ununuzi, andika barua kwa mfanyabiashara mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la bidhaa.


Short answers
5

Andika insha yenye maneno yasiyopungua mia mbili na hamsini (250) na yasiyozidi mia tatu (300) kuhusu umuhimu wa huduma za simu ya mkononi.


Short answers
6

Wewe ni mfanyabiashara mashuhuri mjini Dodoma. Andika barua ya kutuma bidhaa kwa mteja wako aitwaye Dunia Msimbo anayeishi Lindi. Jina lako liwe Nyila Sasisha.


Short answers
7

Andika insha yenye maneno yasiopungua mia mbili (200) na yasiozidi mia tatu (300) kuhusu methali isemayo “Samaki Mkunje angali mbichi”.


Short answers
8

Andaa kadi ya mwaliko kwa rafiki zako ili washiriki katika mahafali ya kumaliza Kidato cha Nne  yatakayofanyika shuleni kwako siku ya Jumamosi tarehe 21/11/2015, kisha kufuatiwa na tafrija fupi
itakayoandaliwa na wazazi wako katika ukumbi wa Kijiji mnamo saa 10.00 jioni. Jina lako liwe Sili
Silali wa SHule ya Sekondari Kiriche.


Short answers
9

Wewe ni Kiranja Mkuu wa Shule ya Sekondari Kazamoyo iliyoko Tanga, jina lako Uwezo Jitihada na unasoma kidato cha nne. Andika barua kwa Mkuu wa Shule ukiomba ruhusa ya kuhudhuria semina ya uelimishaji rika takayofanyika tarehe 10/11/2013 katika Shule ya Sekondari Tutafika iliyoko Moshi. Barua yako ipitie kwa Mwalimu wa Darasa.


Short answers
10

Jifanye wewe una elimu ya kidato cha nne, jina lako Situmai Kasheshe unayeishi kijiji cha Songambele kilichopo wilayani Mpanda. Tumia taarifa zilizomo kwenye tangazo lifuatalo lililotolewa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 01/12/2013 kuandika barua ya maombi ya kazi.
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Kazi : Karani Masijala
Sifa :
● Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu masomo ya Kiingereza na Hisabati
● Awe na umri usiozidi miaka 35
● Awe Mtanzania
● Awe na ujuzi wa kompyuta
Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti na itufikie kabla ya tarehe 15/12/2013.
Maombi yote yatumwe kwa:
Afisa Mwajiri
Kampuni ya Kutengeneza Masufuria
S.L.P 600
KATAVI.


Short answers