Warning: Undefined array key 1 in /home/acaproso/public_html/._System/._Template/.Main.php on line 116
Aina za maneno questions

Aina za maneno questions | form one Kiswahili

Find Aina za maneno examination questions, form one Kiswahili in acaproso.com

# Question
1

Kwa kuzingatia tungo ulizopewa, bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari:
(a) Juzi tulishiriki maandamano ya amani.
(b) Kucheza kwake kunaburudisha.
(c) Kijana mlevi amepata ajali.
(d) Hamisi alikuwa amekwisha kwenda kulima .
(e) Wale vikongwe wamepata msaada.
(f) Mawazo hayo si yangu.
(g) Sitakwenda kwake asilani!
(h) Amekwenda kazini ijapokuwa ni mgonjwa.
(i) Hiki kitawekwa ukumbini.
(j) Mbuzi amekwisha kata kamba.


Short answers
2

Eleza dhima za mofimu "li" kama ilivyotumika katika sentensi zifuatazo:
(a) Shamba letu li kubwa sana.
(b) Wlishelewa kurudi.
(c) Tunalifuatilia.
(d) Limeharibika.
(e) Shikilia.


Short answers
3

Tumia neno “Paa” katika sentensi kuunda dhana zifuatazo:
(a) Nomino
(b) Kitenzi
(c) Kielezi
(d) Kivumishi
(e) Shamirisho


Short answers
4

Onesha nomino katika tungo zifuatazo kisha bainisha ni aina gani ya nomino:
(a) Hatuna budi kumshukuru Mola.
(b) Mazao yamestawi shambani.
(c) Uzalendo usisitizwe shuleni.
(d) Mpeleke mtoto ndani.
(e) Nimechoshwa na upweke.


Short answers