Warning: Undefined array key 1 in /home/acaproso/public_html/._System/._Template/.Main.php on line 116
Matumizi ya sarufi questions

Matumizi ya sarufi questions | form five Kiswahili

Find Matumizi ya sarufi examination questions, form five Kiswahili in acaproso.com

# Question
1

(a) Eleza maana ya viambishi vya O-rejeshi .
(b) Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia O-rejeshi .
(i) Kanu ameleta mpira wa miguu. Ulikuwa unahitajika mpira.
(ii) Rukia anatafuta vitabu. Vitabu vimekwisha.
(iii) Gazeti lilichapwa. Gazeti limekwisha.
(iv) Mtoto ametekwa nyara. Mtoto ameptaikana.
(v) Yule msichana amesimama pale. Yule msichana ni dada yangu.


Short answers
2

Kwa kutumia mifano bainisha kazi mbili za mnyumbuliko na kazi tatu za uambishaji katika lugha
ya Kiswahili.


Short answers
3

Bainisha matumizi ya “ki” iliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:
(i) Kiti kidogo
(ii) A kija apewe mzigo wake
(iii) Kitabu kimechanika
(iv) Kiti kikidogo
(v) Wana kisubiria
(vi) Analima a kiimba
(vii) Atavuna alicho kipanda

(viii) Kitoto hiki sikiwezi
(ix) Aliruka juu kihuni
(x) Anacheza kitoto


Short answers
4

Katika kila tungo zifuatazo taja kielezi na fafanua aina ya kielezi hicho.
(a) Hospitali imefungwa kwa mara ya tatu.
(b) Amekaa juu ya nyumba.
(c) Anapigana kishujaa
(d) Nitaondoka asubuhi na mapema.
(e) Ameelekea upande wa kulia.


Short answers
5

Fafanua dhana zifuatazo kwa kutumia mifano:
(a) Kiunganishi
(b) Mzizi wa neno
(c) Sintaksia
(d) Kitenzi kisaidizi
(e) O-rejeshi.


Short answers