Uandishi questions | form two Kiswahili
Find Uandishi examination questions, form two Kiswahili in acaproso.com
# | Question |
---|---|
1 | Manyanda akiwa mfanyakazi wa kiwanda cha korosho Tanita alipewa taarifa kuhusu ugonjwa wa baba yake. Wewe kama Manyanda andika barua ya kuomba ruhusa. Anuani ya kiwanda ni S.L.P. 1030, Kibaha. Short answers |
2 | Andika insha yenye maneno 250 kuhusu moja ya mada zifuatzo: Short answers |
3 | Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwako, unahitaji marafiki kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo. Andaa kadi ya mwaliko ili kuwapa taarifa rafiki zako. Short answers |
4 | Wewe kama afisa ununuzi, andika barua kwa mfanyabiashara mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la bidhaa. Short answers |
5 | Andika insha yenye maneno yasiyopungua mia mbili na hamsini (250) na yasiyozidi mia tatu (300) kuhusu umuhimu wa huduma za simu ya mkononi. Short answers |
6 | Wewe ni mfanyabiashara mashuhuri mjini Dodoma. Andika barua ya kutuma bidhaa kwa mteja wako aitwaye Dunia Msimbo anayeishi Lindi. Jina lako liwe Nyila Sasisha. Short answers |
7 | Andika insha yenye maneno yasiopungua mia mbili (200) na yasiozidi mia tatu (300) kuhusu methali isemayo “Samaki Mkunje angali mbichi”. Short answers |
8 | Andaa kadi ya mwaliko kwa rafiki zako ili washiriki katika mahafali ya kumaliza Kidato cha Nne yatakayofanyika shuleni kwako siku ya Jumamosi tarehe 21/11/2015, kisha kufuatiwa na tafrija fupi Short answers |
9 | Wewe ni Kiranja Mkuu wa Shule ya Sekondari Kazamoyo iliyoko Tanga, jina lako Uwezo Jitihada na unasoma kidato cha nne. Andika barua kwa Mkuu wa Shule ukiomba ruhusa ya kuhudhuria semina ya uelimishaji rika takayofanyika tarehe 10/11/2013 katika Shule ya Sekondari Tutafika iliyoko Moshi. Barua yako ipitie kwa Mwalimu wa Darasa. Short answers |
10 | Jifanye wewe una elimu ya kidato cha nne, jina lako Situmai Kasheshe unayeishi kijiji cha Songambele kilichopo wilayani Mpanda. Tumia taarifa zilizomo kwenye tangazo lifuatalo lililotolewa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 01/12/2013 kuandika barua ya maombi ya kazi. Short answers |