Uandishi wa barua questions | form one Kiswahili
Find Uandishi wa barua examination questions, form one Kiswahili in acaproso.com
# | Question |
---|---|
1 | Andaa kadi ya mwaliko kwa rafiki zako ili washiriki katika mahafali ya kumaliza Kidato cha Nne yatakayofanyika shuleni kwako siku ya Jumamosi tarehe 21/11/2015, kisha kufuatiwa na tafrija fupi itakayoandaliwa na wazazi wako katika ukumbi wa Kijiji mnamo saa 10.00 jioni. Jina lako liwe Sili Silali wa SHule ya Sekondari Kiriche. Short answers |
2 | Jifanye wewe ni Gudhah Mukish anayeishi mtaa wa Tandamti Gerezani Kariakoo na unataka kuuza gari yako aina ya TOTYOTA CARINA. Andika tangazo kwenye gazeti la Mwananchi. Short answers |
3 | Wewe ni Kiranja Mkuu wa Shule ya Sekondari Kazamoyo iliyoko Tanga, jina lako Uwezo Jitihada na unasoma kidato cha nne. Andika barua kwa Mkuu wa Shule ukiomba ruhusa ya kuhudhuria semina ya uelimishaji rika takayofanyika tarehe 10/11/2013 katika Shule ya Sekondari Tutafika iliyoko Moshi. Barua yako ipitie kwa Mwalimu wa Darasa. Short answers |
4 | Wewe ni mfanyabiashara mashuhuri mjini Dodoma. Andika barua ya kutuma bidhaa kwa mteja wako aitwaye Dunia Msimbo anayeishi Lindi. Jina lako liwe Nyila Sasisha. Short answers |
5 | Jifanye kuwa umepata barua ya mwaliko wa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki yako aitwaye Faraja Matata, itakayofanyika siku ya tarehe 10/10/2012. Kwa bahati mbaya siku tatu kabla ya sherehe umepata safari ya kikazi kuelekea mkoani Singida. Andika barua kumtaarifu rafiki yako kuwa hutaweza kuhudhuria sherehe hiyo. Jina lako liwe Tumaini Baraka. Short answers |
6 | Wewe kama afisa ununuzi, andika barua kwa mfanyabiashara mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la bidhaa. Short answers |
7 | Muundo wa uandishi wa barua za kirafiki na barua za kikazi ni tofauti. Thibitisha kauli hiyo. Short answers |
8 | Manyanda akiwa mfanyakazi wa kiwanda cha korosho Tanita alipewa taarifa kuhusu ugonjwa wa baba yake. Wewe kama Manyanda andika barua ya kuomba ruhusa. Anuani ya kiwanda ni S.L.P. 1030, Kibaha. Short answers |
9 | Muundo wa uandishi wa barua za kirafiki na barua za kikazi ni tofauti. Thibitisha kauli hiyo. Short answers |
10 | Jifanye kuwa umepata barua ya mwaliko wa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki yako aitwaye Faraja Matata, itakayofanyika siku ya tarehe 10/10/2012. Kwa bahati mbaya siku tatu kabla ya sherehe umepata safari ya kikazi kuelekea mkoani Singida. Andika barua kumtaarifu rafiki yako kuwa hutaweza kuhudhuria sherehe hiyo. Jina lako liwe Tumaini Baraka Short answers |