Warning: Undefined array key 1 in /home/acaproso/public_html/._System/._Template/.Main.php on line 116
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi questions

Uhakiki wa kazi za fasihi andishi questions | form three Kiswahili

Find Uhakiki wa kazi za fasihi andishi examination questions, form three Kiswahili in acaproso.com

# Question
1

Kwa kutumia tamthiliya m bili (2) kati ya hizo zilizoorodheshwa, jadili jinsi kazi za wasanii hao zilivyochangia katika ujenzi wa jamii.

Tamthiliya
Mfalme Juha ………………………. F. Topan (DUP)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe …………….. E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu ………………………. Medical Aid Foundation (TPH)


Long answers
2

“Matendo yasiyo na utu hujadiliwa na wasanii”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia riwaya mbili (2) kati ya hizo zilizoorodheshwa.

Riwaya
Kusadikika ………………………. S. Robert (E.P.)
Watoto wa Mama N’tilie ………………………. E. Mbogo (H.P.)
Kiu ya Haki ………………………. Z. Mwanga (R.P.)


Long answers
3

“Mwandishi wa fasihi ni mchunguzi wa jamii ambaye huyaweka wazi maovu mbalimbali”. Jadili
jinsi kazi za washairi wawili kati ya hao walioorodheshwa zilivyosadifu kauli hii.

Ushairi
Diwani ya Mloka ………………………. C. Mloka (B.P.)
Malenga Wapya ………………………. TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka ………………………. T.A. Mvungi (EP & DLTD)


Long answers
4

“Mshairi ni mhakiki wa jamii”. Kwa kutumia vitabu teule v iwili (2) vya ushairi ulivyosoma, jadili kauli hii.

Ushairi
Diwani ya Mloka C. Mloka (B.P)
Malenga Wapya TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka T. A. Mvungi (EP & DLTD)


Long answers
5

“Jina la kitabu ni kivutio cha wasomaji wa riwaya”. Kwa kutumia riwaya teule m bili (2) ulizosoma linganisha majina ya vitabu jinsi yanavyosadifu yaliyomo.

Riwaya
Kusadikika S.Robert (E.P)
Watoto wa Mama N’tilie E.Mbogo (H.P)
Kiu ya Haki Z.Mwanga (R.P.)


Long answers
6

“Waandishi wengi huandika kazi zao kwa lengo la kutoa ujumbe katika jamii”. Kwa kutumia
tamthiliya mbili (2) zilizoorodheshwa, thibitisha ukweli wa kauli hii.

Tamthiliya
Mfalme Juha F.Topan (DUP)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E.Semzaba (ESC)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation (TPH)


Long answers
7

Linganisha na linganua miundo iliyotumiwa na waandishi wa shairi mbili (2) ulizosoma kati ya
hizo zilizoorodheshwa.

Ushairi
Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya TAKILUKI(DUP)
Mashairi ya Chekacheka T.A. Mvungi (EP & DLTD)


Long answers
8

Lugha anayoitumia mwandishi katika kazi yake ya fasihi ndiyo inayosaidia katika kufikisha wazo lake kwa hadhira. Kwa kutumia riwaya teule mbili (2) ulizosoma, jadili jinsi wasanii wa riwaya hizo walivyotumia kipengee cha tamathali za semi.

Riwaya
Takadini Ben Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N’tilie E.Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu A.J. Safari (H.P)


Long answers
9

Jadili kufaulu na kutofaulu kimaudhui kwa waandishi wawili (2) wa tamthiliya teule ulizosoma.

Tamthiliya
Orodha Steve Raynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E.Semzaba (ESC)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation (TPH)


Long answers
10

“Kiongozi katika jamii ni nahodha ambaye hutakiwa aongoze chombo kisiende mrama.” Kwa
kutumia hoja tatu (3) kutoka katika kila diwani jadili kauli hii ukitumia wasanii wawili uliowasoma.

ORODHA YA VITABU
Ushairi
Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka T.A. Mvungi (EP & D. LTD)
Riwaya
Takadini Ben Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N’tilie E.Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu A.J. Safari (H.P)
Tamthiliya
Orodha Steve Raynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E.Semzaba (ESC)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation (TPH)


Long answers