Primary and secondary education past papers.

STANDARD 4-SCIENCE-2019-NATIONAL EXAM-TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE

05   SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda : Saa 1:30      Alhamisi, 21 Novemba 2019 asubuhi

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali matano (5).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizotolewa katika kila swali.
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  5. Simu za mkononi na vitu vingine visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Jina na Namba yako ya upimaji katika nafasi iliyo kwenye sehemu ya juu ya kila ukurasa.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU
Namba ya Swali Alama Saini ya Mtahini Saini ya Mhakiki
1      
2      
3      
4      
5      
Jumla      

 



SEHEMU A(Alama 30)

Jibu maswali yote katika sehemuhii.

  1. Jibu kipengele (i)-(v) kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuandika katika kisanduku.

(i) Chakula salama ni kile ambacho

  1. kimepuliziwa dawa ya kuua wadudu.
  2. kimehifadhiwa katika chombo safi
  3. kimehifadhiwa kwa muda mfupi
  4. kimehifadhiwa mahali penye mwanga

(ii) Zifuatazo ni njia za kujikinga dhidi ya magonjwa isipokuwa

  1. kufunika mdomo wakati wa kukohoa
  2. kulala mahali safi na salama
  3. kunywa maji safi na salama
  4. kunawa mikono kabla ya kwenda chooni

(iii) Magonjwa yapi hutokana na uchafuzi wa vyanzo vya maji?

  1. Kifaduro na surua
  2. UKIMWI na kipindupindu
  3. Malaria na trakoma
  4. Kipindupindu na kichocho

(iv) Nini kazi ya mate katika mmeng`enyo wa chakula?

  1. Kulainisha chakula
  2. Kulainisha mdomo
  3. Kulainisha meno
  4. Kulainisha ulimi

(v) Mmeng`enyo wa chakula huanza katika sehemu ipi katika mfumo?

  1. Tumboni
  2. Kwenye umio
  3. Kinywani
  4. Katika kongosho.

  1. Jibu vipengele (i)-(iv), kwa kuoanisha maelezo katika Orodha A na hali za maada katika Orodha B. Andika herufi ya jibu katika mabano uliyopewa.
Orodha A Herufi Orodha B
(i)Hali ya maada nyepesi zaidi. (    )
  1. Gesi
  2. Soda
  3. Mvuke
  4. Kimiminika
  5. Chembechembe
  6. Chaki
  7. Yabisi
(ii) Hali ya maadda yenye umbo maalumu. (    )
(iii) Mfano wa maada katika hali yabisi. (    )
(iv) Maada inayochukua umbo la chombo. (    )
(v)Mfano wa maada katika hali ya gesi.  (    )

 


  1. Jibu vipengele (i)-(v) kwa kuchagua neno sahihi kutoka kwenye kisanduku na kuliandika kwenye nafasi uliyopewa.
Kiungulia, kuvimbiwa, unyafuzi, kukosa choo, meno kuuma, vidonda vya tumbo, mwozo wa meno.

(i)Hali ya kupata kinyesi kigumu na chenye mkauko huitwa …..

(ii) Hali inayosababishwa na kujaa kwa gesi nyingi katika tumbo huitwa …..

(iii) Hali ya kuhisi maumivu ya kuungua katika umio na kifua inaitwaje? …..

(iv) Katikamfumo wa chakula, michubuko ndani ya kuta za tumbo huitwa …..

(v) Ni madhara gani yatatokea katika meno kutokana na ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi? ….


SEHEMU B(Alama 20)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Soma habari ifuatayo kisha jibu vipengele (i)- (v).

Aina nyingi za vyakula tunavyotumia katika maisha yetu ya kila siku huwa vimepikwa. Chakula hupikwa kwa kutumia nishati ya joto. vifaa vinavyotumikakuwezesha upikaji wa vyakula vyetu huitwa majiko. Nchini Tanzania, aina ya majoko yanayotumiwa zaidi ni ya kuni na mkaa. Kwa miaka ya karibuni, kumekuwa na ongezeko la watumiaji wa majiko ya gesi katika maeneo ya mijini na vififni. Uchaguzi wa aina ya joko hutofautina kulingana na upatikanaji, gharama na usalama wa aina ya fueli inayotumika. Hayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati wa uchaguzi wa aina ya jiko la kutumia.

(i) Taja aina mbili za majiko yanayotumiwa na watu wengi Tanzania _____

(ii) Ni aina gani ya nishati hutmika kupikia ? _______

(iii) Je, ni kitu gani kinatumika kutofautisha aina za majiko? _______

(iv) Unafikiri ni kwanini watu wengi hutumia majiko ya kuni? _____

(v) Taja aina nyingine mbili za majiko tofauti naliyotajwa katika habari uliyosoma. ____


  1. Chunguza picha uliyopewa kisha jibu vipengele (i)-(v).

Sayansi na teknolojia

(i) kifaa kilichooneshwa kwenye picha kinaitwaje? ……..

(ii) Onesha sehemu inayosafirisha nishati kutoka kwenye soketi kwa kutumia herufi A.

(iii) Onesha sehemu inayoonesha picha kwa kutumia herufi B.

(iv) Onesha sehemu inayodaka mawimbi kwa kutumia herufi C.

(v) Kwanini kifaa kilichooneshwa kwenye picha ni muhimu kwetu?


News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-10-07: questions

Questions Uploaded on 2024-10-07


questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02


questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29