Primary and secondary education past papers.

STANDARD 4-SOCIAL STUDIES-2019-NATIONAL EXAM-TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE

03   MAARIFA YA JAMII

Muda : Saa 1:30      Alhamisi, 21 Novemba 2019 mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali manne (4).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizotolewa katika kila swali.
  4. Majibu yote yaandikwe kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  5. Simu za mkononi na vitu vingine visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Jina na Namba yako ya upimaji katika nafasi iliyo kwenye sehemu ya juu ya kila ukurasa.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU
Namba ya Swali Alama Saini ya Mtahini Saini ya Mhakiki
1      
2      
3      
4      
Jumla      

 



SEHEMU A (Alama 28)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Jibu kipengele cha (i) – (viii) kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuiandika katika kisanduku.

(i) Bibi na Bwana Juma wana mtoto aitwaye Neema ambaye aliolewa na kuzaa mtoto aitwaye Yusufu. Bwana Juma ni nani kwa Yusufu?

  1. Baba
  2. Babu
  3. Mjomba
  4. Mpwa

(ii) Ipi ni faida ya kiafya waipatayo wanafunzi kwa kucheza ngoma za kitamaduni?

  1. Kuendeleza utamaduni
  2. Kupata hamasa ya kufanya kazi
  3. Kupata zawadi mbalimbali
  4. Kufanya mwili uwe imara na afya

(iii) Bwana na Bibi James walioana mwaka 2014. Hawajafanikiwa kupata mtoto mpaka sasa. Hii familia inaitwaje?

  1. Ya awali
  2. Ya watoto yatima
  3. Ya mke na mme
  4. Ya makubaliano

(iv) Kipi kati ya vifuatavyo ni kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania/

  1. Ubinafsishaji wa viwanda
  2. Ujenzi wa viwanda
  3. Elimu bure kwa watanzania wote
  4. Uanzishaji wa vyama vingi vya siasa

(v) Ni kiongozi yupi katika Tanzania hupigiwa kura na mwananchi kila baada ya miaka mitano?

  1. Jaji mkuu
  2. Raisi
  3. Spika wa bunge
  4. Waziri Mkuu

(vi) Bwana John anamiliki mashamba makubwa ambayo huyakodisha kwa watu. Hii ni aina gani ya ukabaila?

  1. Ubugabire
  2. Ntemi
  3. Nyarubanja
  4. Ujima

(vii) Ni mawaziri wakuu wangapi walifanya kazi katika serikali ya awamu ya kwanza ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

  1. Wanne
  2. Moja
  3. Watatu
  4. Wawili

(viii) Mfumo upi wa uzalishaji mali ulishamiri katika sehemu ya magharibi mwa Tanzania?

  1. Ujima
  2. Ubugabire
  3. kihamba
  4. Umwinyi

  1. Jibu kipengele cha (i) – (vi) kwa kuonanisha maneno yenye madini mbalimbali katika Fungu A na aina za madini yanayopatikana katika Fungu B. Andika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano uliyopewa.
Fungu A Herufi Fungu B
(i) Geita mkoa wa Geita ( )
  1. Almasi
  2. Bati
  3. Chumvi
  4. CHuma
  5. Dhahabu
  6. Chokaa
  7. Makaa ya mawe
  8. Tanzanaiti
(ii) Uvinza mkoa wa Kigoma ( )
(iii) Liganga mkoa wa Njombe ( )
(iv) Mererani mkoa wa Arusha ( )
(v) Karagwe mkoa wa kagera ( )
(vi) Mwadui mkoa wa shinyanga ( )

 


SEHEMU B (Alama 22)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuandika jibu sahihi katika  nafasi iliyoachwa wazi.

Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyomzunguka mwanadamu.Mazingira hujumuisha watu, miti, wanyama pamoja na vitu vingine .Kwa ujumla, mazingira hujumuisha vitu vilivyo hai na visivyo hai.

Mazingira ya shule huundwa na vitu vilivyo hai na visivyo hai. Mifano ya vitu vilivyohai vinavyopatikana katika mazingira ya shule ni binadamu na mimea. Vitu visivyo hai vinavyopatikana katika mazingira ya shule ni samani, vitabu, chaki, kalamu na wino, kalamu za risasi na vifutio vya ubao. Samani hujumuisha meza, dawati, viti na kabati. Vitu vyote vyenye uhai na visivyo na uhai vinavyopatikana katika mazingira ya shule yetu ni muhimu hivyo tunapaswa kuvitunza.

Maswali

(i) Kitu chochote kinachomzunguka binadamu huitwa …….

(ii) Kipi kati ya mimea na samani ni kitu kisicho na uhai? ….

(iii)Mifano miwili ya vitu hai vinavyopatikana katika mazingira ya shule ni binadamu na …..

(iv) Vitu visivyo hai ambavyo hupatikana katika mazingira ya shule ambavyo hutumika katika kuandika na kuchorea ni kalamu ya wino, chaki na ……….

(v) Kwa nini tunatunza vitu vilivyo hai na visivyo hai? ……..

(vi) Kipi kati ya kabati na chaki ni mfano wa samani? …..

(vii) Mbali na kundi la viumbe hai, kundi gani jingine linalopatikanaa katika mazingira ya shule? ...

 


  1. Soma mchoro wa pande kuu nne za dunia uliopewa kisha jibu kipengele cha (i) – (iv) kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.

Maarifa ya jamii darasa la nne

(i) Kikombe kipo upande gani wa dira ya dunia?

(ii) Taja upande wa dunia wenye penseli

(iii) Kiti kipo upande gani wa dira ya dunia?

(iv) Upande wa dunia ambao jua linachomoza umewakilishwa na kitu gani?


News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-10-07: questions

Questions Uploaded on 2024-10-07


questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02


questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29