Primary and secondary education past papers.

STANDARD 4-SCIENCE-2018-NATIONAL EXAM-TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE

05   SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda : Saa 1:30      Ijumaa, 23 Novemba 2018 asubuhi

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali matano (5).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizotolewa katika kila swali.
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  5. Simu za mkononi na vitu vingine visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Jina na Namba yako ya upimaji katika nafasi iliyo kwenye sehemu ya juu ya kila ukurasa.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU
Namba ya Swali Alama Saini ya Mtahini Saini ya Mhakiki
1      
2      
3      
4      
5      
Jumla      

 



SEHEMU A (Alama 30)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Jibu kipengele (i) – (v) kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuandika kwenye kisanduku.

(i) Lipi ni kundi la viube hai pekee?

  1. Jani, ndege na jiwe
  2. Paka, mti na kuku
  3. Mti, jani na mbao
  4. Kiti, jani na ndege

(ii) Gesi ya oksjeni husaidia kuunguza chakula ili kupata

  1. nishati
  2. moshi
  3. mvuke
  4. hewa

(iii) Kwanini ni muhimu kusafisha miili yetu?

  1. Ilikuzuia magonjwa
  2. Ili kupaka mafuta
  3. Ili kupendezesha ngozi
  4. Ili kuupa mwili hewa.

(iv) Yapi ni madhara ya uharibifu wa mazingira?

  1. Kupotea kwa wadudu
  2. kusambaa kwa mavumbi
  3. kuongezeka kwa wanyama
  4. kutokea kwa magonjwa

(v) Maji yana umuhimu gani kwa viumbe hai?

  1. Kusafirisha virutubisho
  2. Kutengeneza chakula
  3. Kuyeyusha virutubisho
  4. Kutuliza kiu

  1. Jibu kipengele (i) – (v) kwa kuoanisha maelezo kuhusu sehemu za runinga katika orodha A na sehemu za runinga katika orodha B. Andika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano uliyopewa.
Orodha A Jibu Orodha B
(i) Sehemu inayoonesha picha na maandishi (  )
  1. Rimoti
  2. Vitufe
  3. Switchi
  4. Waya
  5. Spika
  6. Antena
  7. Sikirini
(ii) Sehemu inayotoa sauti kwenye runinga ili kupata ujumbe. (  )
(iii) Sehemu ya kuamrishia runinga kwa mbali (  )
(iv) Sehemu inayodaka mawimbi ya runinga angani (  )
(v) Sehemu inayosafirisha umeme kutoka kwenye soketi hadi kwenye runinga. (  )

 


  1. Jibu kipengele (i) – (v) kwa kuchagua neno sahihi kutoka kwenye kisanduku na kuliandika kwenye nafasi uliyopewa.
chaja, laini ya simu, sikirini, antena, kipaza sauti, betri

(i) Sehemu gani hutumika kuonyesha majina na namba kwenye simu?

(ii) Sehemu inayopokea mawimbi ya sauti na picha inajulikana kama ….

(iii) Sehemu inayoingiza nguvu ya umeme kwenye simu inaitwaje?

(iv) Sehemu gani inahifadhi nishati ya umeme kwenye simu ?

(v) Sehemu gani hutumika kuunganisha simu na mtandaowa simu?


SEHEMU B ( Alama 20)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Umepewa hatua A- E za ufuaji wa soksi.Panga hatua hizo kwa mtiririko kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho kwa kuandika sentensi ya hatua husika katika nafasi ya kujibia uliyopewa.
  1. Zisuuze soki katika maji safi kuondoa sabuni
  2. Fikicha sehemu za juu na chini za soksi
  3. Anika soksi kwenye kamba ili zikauke.
  4. Ziweke soksi kwenye beseni la maji safi na pakaa sabuni.
  5. Andaa maji safi na sabuni.
Hatua Herufi
Hatua ya 1  
Hatua ya 2  
Hatua ya 3  
Hatua ya 4  
Hatua ya 5  

 


  1. Chunguza picha zifuatazo kisha jibu maswali katika kipengele (i) – (v).

Kichocho sayansi darasa la nne

(i) Taja shughuli inayofanywa na watu wawili wanaoelea kwenye maji.

(ii) Tofauti na binadamu, ni mnyama gani mwingine anaelea kwenye maji?

(iii) Ni ugonjwa gani unaweza kuenezwa na mnyama anaeyeelea  katika maji?

(iv) Taja dalilimbili za ugonjwa ulioutaja.

(v) Ogani gani za mwili hushambuliwa na ugonjwa huo?


News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-10-07: questions

Questions Uploaded on 2024-10-07


questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02


questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29