Uandishi questions | form two Kiswahili

(2658) Question Category: Short answers

Wewe ni mfanyabiashara mashuhuri mjini Dodoma. Andika barua ya kutuma bidhaa kwa mteja wako aitwaye Dunia Msimbo anayeishi Lindi. Jina lako liwe Nyila Sasisha.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2659) Question Category: Short answers

Andika insha yenye maneno yasiopungua mia mbili (200) na yasiozidi mia tatu (300) kuhusu methali isemayo “Samaki Mkunje angali mbichi”.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2660) Question Category: Short answers

Andaa kadi ya mwaliko kwa rafiki zako ili washiriki katika mahafali ya kumaliza Kidato cha Nne  yatakayofanyika shuleni kwako siku ya Jumamosi tarehe 21/11/2015, kisha kufuatiwa na tafrija fupi
itakayoandaliwa na wazazi wako katika ukumbi wa Kijiji mnamo saa 10.00 jioni. Jina lako liwe Sili
Silali wa SHule ya Sekondari Kiriche.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2661) Question Category: Short answers

Wewe ni Kiranja Mkuu wa Shule ya Sekondari Kazamoyo iliyoko Tanga, jina lako Uwezo Jitihada na unasoma kidato cha nne. Andika barua kwa Mkuu wa Shule ukiomba ruhusa ya kuhudhuria semina ya uelimishaji rika takayofanyika tarehe 10/11/2013 katika Shule ya Sekondari Tutafika iliyoko Moshi. Barua yako ipitie kwa Mwalimu wa Darasa.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2662) Question Category: Short answers

Jifanye wewe una elimu ya kidato cha nne, jina lako Situmai Kasheshe unayeishi kijiji cha Songambele kilichopo wilayani Mpanda. Tumia taarifa zilizomo kwenye tangazo lifuatalo lililotolewa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 01/12/2013 kuandika barua ya maombi ya kazi.
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Kazi : Karani Masijala
Sifa :
● Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu masomo ya Kiingereza na Hisabati
● Awe na umri usiozidi miaka 35
● Awe Mtanzania
● Awe na ujuzi wa kompyuta
Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti na itufikie kabla ya tarehe 15/12/2013.
Maombi yote yatumwe kwa:
Afisa Mwajiri
Kampuni ya Kutengeneza Masufuria
S.L.P 600
KATAVI.

Answer / Solution

UNSOLVED


View All Topics
News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02


questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29


questions

2024-03-19: questions

Questions Uploaded on 2024-03-19

Dismissible in 10 seconds