Ufahamu na ufupisho questions | form five Kiswahili

(4800) Question Category: Ufahamu

Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu kwa usahihi maswali yanayofuata.
Vitabu ni rafiki kwa wanadamu. Viko chini ya amri siku zote. Ukurasa wa kitabu kilichopigwa
chapa ni usemi bora usiotoweka maishani. Huwapa mafundisho na faida kubwa watu
wazingatiapo. Vitabu ni hazina bora kuliko hazina ya mfalme yeyote katika dunia hii. Ni
machimbo azizi ya usanifu, maandiko, ujuzi na maarifa. Kitabu kizuri ni rafiki, mwalimu na
kiongozi wa watu katika maisha.
Iliwapasa babu zetu kwenda safari kubwa kusikiliza maneno ya mtu mwenye hekima. Sasa
hekima imo katika vitabu mezani petu inatungoja. Kwa kweli, kuna vitabu vingi sana. Husemwa
kwamba kuna vitabu vya kitambo, tusomavyo kisha tukavitupa. Kuna vitabu vya nyakati zote,
tupendavyo kusoma mara kwa mara, kama mpenzi asomavyo mara kwa mara barua ya kipenzi
chake. Hivyo, katika wakati huu uliojaa vitabu vizuri ni vibaya, uchaguzi wa vitabu ni mashaka
makubwa. Tusiharibu wakati wetu ujao kwa kitabu chochote hafifu, ambacho sifa yake kubwa ni
jina zuri na jalada la kupendeza tu, “nyumba nzuri si mlango, fungua uingie ndani.”
Imesemwa kwamba vitabu fulani vinapaswa kujaribiwa, yaani tupekue kurasa zake na tutazame
yaliyomo, baadhi yake lazima yamezwe, yaani visomwe vyote toka jalada hata jalada na vingine
vichache vimebidi kutafunwa na kuyeyushwa, yaani visomwe mara kwa mara. Ni bora kusoma
kwa kujifundisha kuliko kwa kujiburudisha, ingawa kusoma kwa kujiburudisha kuna manufaa
yake, hasa kwa mtu mwenye kazi ngumu. Kuna vitabu bora vya zamani na vya sasa vya kusoma
vilevile. Swali tunalojiuliza visomwe vipi? Rai iliyotolewa ni kwamba ili kupata ujuzi, lazima
tusome vitabu vipya kabisa, pia twaweza kusoma vitabu vya zamani kabisa ila kwa jicho la
uhakiki. Ila kuna usemi usemao “ukitaka kumficha mjinga mpe kitabu.”
Vitabu vibaya vikiingia mikononi mwa vijana, akili zao huambukizwa na maongozi yake maovu.
Vijana wengi hodari wameangamia, kwa sababu ya kusoma vitabu vibaya. Vitabu vizuri
hutakasa , hukuza tena hustawisha akili, hujenga na tabia yetu. Vitabu vya historia hutia busara,
mashairi huleta akili na hesabu huongeza werevu. Lakini kila mtu kila mtu akubali kwamba
kusoma kunamsitawisha mtu.
Faida nyingine ya kusoma vitabu ni kwa mtu hasa aliyeacha masomo yake ya desturi, kwake
vitabu ni aendeleo ya elimu. Aweza kufululiza masomo yake nyumbani. Kitabu kizuri ni rafiki
bora kabisa atakuongoza peponi .
Maswali
(a) Andika kichwa cha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyozidi matano.
(b) Eleza mawazo makuu mawili ya mwandishi.

(c) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari hii.
(i) Hazina
(ii) Kitambo
(iii) Hutakasa
(iv) Peponi
(d) Mwandishi anaposema “nyumba nzuri si mlango, fungua uingie ndani” anamaanisha nini?”
(e) Nini maana ya usemi “ukitaka kumficha mjinga mpe kitabu.”
(f) Ili tuweze kupata maarifa, mwandishi anashauri tusome vitabu gani?

Answer / Solution

UNSOLVED

(4801) Question Category: Ufahamu

Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu kwa usahihi maswali yanayofuata.
Vitabu ni rafiki kwa wanadamu. Viko chini ya amri siku zote. Ukurasa wa kitabu kilichopigwa
chapa ni usemi bora usiotoweka maishani. Huwapa mafundisho na faida kubwa watu
wazingatiapo. Vitabu ni hazina bora kuliko hazina ya mfalme yeyote katika dunia hii. Ni
machimbo azizi ya usanifu, maandiko, ujuzi na maarifa. Kitabu kizuri ni rafiki, mwalimu na
kiongozi wa watu katika maisha.
Iliwapasa babu zetu kwenda safari kubwa kusikiliza maneno ya mtu mwenye hekima. Sasa
hekima imo katika vitabu mezani petu inatungoja. Kwa kweli, kuna vitabu vingi sana. Husemwa
kwamba kuna vitabu vya kitambo, tusomavyo kisha tukavitupa. Kuna vitabu vya nyakati zote,
tupendavyo kusoma mara kwa mara, kama mpenzi asomavyo mara kwa mara barua ya kipenzi
chake. Hivyo, katika wakati huu uliojaa vitabu vizuri ni vibaya, uchaguzi wa vitabu ni mashaka
makubwa. Tusiharibu wakati wetu ujao kwa kitabu chochote hafifu, ambacho sifa yake kubwa ni
jina zuri na jalada la kupendeza tu, “nyumba nzuri si mlango, fungua uingie ndani.”
Imesemwa kwamba vitabu fulani vinapaswa kujaribiwa, yaani tupekue kurasa zake na tutazame
yaliyomo, baadhi yake lazima yamezwe, yaani visomwe vyote toka jalada hata jalada na vingine
vichache vimebidi kutafunwa na kuyeyushwa, yaani visomwe mara kwa mara. Ni bora kusoma
kwa kujifundisha kuliko kwa kujiburudisha, ingawa kusoma kwa kujiburudisha kuna manufaa
yake, hasa kwa mtu mwenye kazi ngumu. Kuna vitabu bora vya zamani na vya sasa vya kusoma
vilevile. Swali tunalojiuliza visomwe vipi? Rai iliyotolewa ni kwamba ili kupata ujuzi, lazima
tusome vitabu vipya kabisa, pia twaweza kusoma vitabu vya zamani kabisa ila kwa jicho la
uhakiki. Ila kuna usemi usemao “ukitaka kumficha mjinga mpe kitabu.”
Vitabu vibaya vikiingia mikononi mwa vijana, akili zao huambukizwa na maongozi yake maovu.
Vijana wengi hodari wameangamia, kwa sababu ya kusoma vitabu vibaya. Vitabu vizuri
hutakasa , hukuza tena hustawisha akili, hujenga na tabia yetu. Vitabu vya historia hutia busara,
mashairi huleta akili na hesabu huongeza werevu. Lakini kila mtu kila mtu akubali kwamba
kusoma kunamsitawisha mtu.
Faida nyingine ya kusoma vitabu ni kwa mtu hasa aliyeacha masomo yake ya desturi, kwake
vitabu ni aendeleo ya elimu. Aweza kufululiza masomo yake nyumbani. Kitabu kizuri ni rafiki
bora kabisa atakuongoza peponi .

Swali;

Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno mia moja na ishirini .

Answer / Solution

UNSOLVED

(4810) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Waafrika ni binadamu ambao wamepitia mateso na shida nyingi sana. Baadhi ya mateso
yalisababisha kumwaga damu na kutoa uhai na kibaya zaidi yalisababisha kupotea kwa tutu na
asili ya mwafrika. Wengine walithubutu kusema kuwa waafrika wana laana na jitihada zozote za
kujaribu kuwakomboa ni kama kufuru .
Waafrika walinyanyaswa ndani ya ardhi yao wenyewe, walifungwa minyororo na kuuzwa kama
bidhaa sokoni. Walitumikishwa katika mashamba na migodi kwa ujira mdogo. Magonjwa
yakawaandama na njaa ikawatafuna watu weusi bila huruma. Waliletewa silaha za kuuana
wenyewe kwa wenyewe, madhehebu na makabila vikawa chanzo cha mapigano. Watu weusi
wakabaki katika hali tete ambayo haikuchachusha tafakuri zenye kuleta maendeleo, kwa sababu
taharaki ilitawala jamii.
Ndani ya uhuru wa bendera, wakapandikiziwa viongozi ambao hawakutofautiana na ile hadithi ya
Kimbwangai nyani aliyetolewa mkia ili afanane na binadamu. Walipata fursa lakini hawakutenda
ya kuwanufaisha wananchi wao. Hayo yalitendeka si kwa sababu kuwa watu weusi si viumbe
razini la hasha! Yalitokana na shinikizo la mabepari waliotaka kupata malighafi ili kuneemesha
kasri zao kiuchumi.
Katika enzi hizi za utandawazi, nchi za Afrika zimekuwa soko kubwa la bidhaa za nchi tajiri,
zenye viwanda vinavyotegemea malighafi toka Afrika. Mitumba huletwa na kuuziwa wananchi
kwa bei nafuu jambo linalohatarisha mazingira. Uwekezaji katika sekta ya madini umeshamiri na
umekuwa tishio kubwa kwa ustawi wa jamii, twabakia na ardhi yenye mashimo.
Kwa ujumla waafrika wanakabiliwa na umaskini uliotopea kwa kipindi kirefu. Wakati umefika
sasa wa kulipwa deni, hatuhitaji malipo ya fadhila, pesa wala maneno matamu. Malipo ya
thamani yatakayokubalika na kizazi hiki na kizazi kijacho ni kuwaacha watu weusi kuwa huru
katika nyanja zote za maisha, ili wajenge upya jamii zao:

Maswali

  1. (a) Toa maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyoisoma:
    (i) Kufuru
    (ii) Ujira
    (iii) Tafakuri
    (iv) Taharaki
    (v) Fursa
    (vi) Kasri
    (vii) Mitumba
    (viii) Uliotopea
    (b) Mwandishi ana maana gani anaposema “hawakutofautiana na ile hadithi ya Kimbwangai nyani aliyetolewa mkia ili afanane na binadamu.” 

          (c) Unaelewa nini kuhusu uhuru wa bendera, toa maelezo yasiyozidi mistari mitatu.

          (d) Kwa kurejea aya ya nne (4), mwandishi ana mtazamo gani kuhusu utandawazi kwa nchi
           za Afrika.

  1. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno mia moja (100).

Answer / Solution

UNSOLVED

View All Topics
News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02

questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29

questions

2024-03-19: questions

Questions Uploaded on 2024-03-19

Dismissible in 10 seconds