Ufahamu questions | form four Kiswahili

(2591) Question Category: Ufahamu

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kando ya namba ya swali.
Nisubiri! Nisubiri nini? Sikupewa talaka. Nilitelekezwa. Jani linapeperushwa lakini hakuna mkono wowote unaothubutu kuliokota, kama vile ambavyo angesema nyanya yangu.
Hata hivyo niliishi. Niliyajua matatizo ya usafiri yaliyokuwepo. Wanangu walikwenda shuleni kwa taabu lakini walivumilia na kuchekelea. Siku moja nikamsikia dada akiwashauri. "Hasa! Msimwambie mama jinsi watu wanavyobanana mwenye magari wakati wa kwenda na kurudi kazini".
Nililia kwa furaha iliyochanganyika na huzuni. Nilifurahi kwa vile nilipendwa na wanangu na
nilihuzunika kwa vile sikuwa na uwezo wa kuikabili hali halisi iliyokuwepo. Kwa hiyo nilikueleza bila kukuficha hali hiyo ya kuhuzunisha ya maisha yetu. Wakati ambapo bibi mamamkwe alikuwa akizitembelea pembe zote za mji akitumia gari la Modu, na Binetuu alikuwa akitamba katika barabara zote akiendesha gari la aina ya Alfa Romeo, mara jekundu mara jeupe.
Sitasahau kamwe jamala uliyonifanyia wewe, dada yangu. Wala sitasahau kamwe furaha na mshangao nilioupata wakati ambapo muuzaji wa magari ya aina ya Fiat aliponiita na kuniambia nichague gari nililotaka, na kwamba wewe ungegharimia kila kitu. Wanangu walishangilia kwa furaha walipotambua kwamba mahangaiko yao yalikuwa karibu kumalizika, mahangaiko wayapatayo wanafunzi wengi sana kila siku.
Katika urafiki, mna upendo mkuu usiojulikana. Huwa unakomaa wakati wa matatizo. Lakini ukali uliozidi mno huua upendo. Urafiki hukaa imara katika nyakati zinazochosha na kuudhi na kuwatenganisha waliooana. Ama kwa hakika katika urafiki mna upendo uliolenga juu kabisa kusikojulikana. Wewe sonara ulijinyima na ukaweza kunisaidia wakati wa dhiki.
Nikajifunza kuendesha na nikautawala woga wangu. Hii nafasi ndogo iliyoko kati ya usukani na kiti cha mbele ikawa yangu. Ninapokanyaga klachi mwendo unaongezeka. Nikikanyaga breki mwendo unapungua, na ninapotaka kwenda kasi nakanyaga akselereta. Nilijivunia akselereta. Nilipoikanyaga kidogo tu gari ilichanganya mwendo mkali. Miguu yangu ikajifunza kuchezecheza juu ya hizo pedali. Wakati nilipokuwa nimekata tamaa kabisa nilikuwa najisemea mwenyewe: "Kwa nini Binetuu aendeshe gari na siyo mimi? Tena niliwaza." Nisimdanganye Aisatu! Niliishinda hiyo vita ya mishipa ya fahamu na ya kujishinda binafsi. Niliipata leseni ya kuendesha na nilikufahamisha.
Nilikueleza, na sasa je? Wanangu wakiwa wamestarehe kwenye kiti cha nyuma ya gari yangu aina ya Fiat 125, rangi ya maziwa, ambayo uliniletea wanaweza kumwangalia kwa dharau yule mke mwenzangu.

Maswali
(i) Mwandishi wa habari hii ana matatizo ya
A kupewa talaka na mumewe
B umaskini uliokithiri
C kutelekezwa na mumewe
D kutokuwa na usafiri
E kuwa na watoto wengi.
(ii) Binetuu ni
A rafiki yake mwandishi
B bibi mkwe wake mwandishi
C mke mwenzie mwandishi
D hawana uhusiano wowote
E jirani wa mwandishi.
(iii) Mwandishi anaposema “katika urafiki mna upendo mkuu … unakomaa wakati wa matatizo”,
anamaanisha kuwa
A akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli
B rafiki wa kweli ni yule anayekupenda wakati wa dhiki tu
C kila shetani na mbuyu wake
D huruma ya kweli inapatikana wakati wa dhiki
E rafiki ni yule mwenye upendo wa chati.
(iv) Nyanya kama lilivyotumiwa na mwandishi maana yake ni
A tunda linaloungwa kwenye mboga B rafiki mzee
C mama wa mzazi wako D ajuza
E yote si kweli.
(v) Kulingana na habari hii kuna vitu vitatu muhimu vinavyotumika wakati wa kuendesha gari.
Navyo ni:
A Usukani, breki na klachi
B Kiti cha dereva, klachi na akselereta
C Pedali, klachi na breki
D Klachi, akselereta na breki
E Akselereta na breki.
(vi) Neno “jamala” kama ilivyotumiwa na mwandishi linamaanisha
A wema wako B juhudi zako
C rehema zako D upendo wako
E upole wako.
(vii) Kulingana na habari hii Modu ni
A jina la mume wa mwandishi
B aina ya gari
C halijulikani maana yake
D majibu yote si kweli
E ni rafiki wa sonara.

(viii) Rafiki yake mwandishi kazi yake ni
A sonara
B mfanyabiashara
C muuza magari
D afisa
E dereva.
(ix) Sifa za watoto wa mwandishi kulingana na habari hii ni
A wenye upendo, huruma, wavumilivu na wapole
B wavumilivu na wenye furaha wakati wote
C wakaidi na wanaocheka ovyo
D wakaidi kwa majirani na marafiki
E sifa zote hizo wanazo.
(x) Mwandishi anazungumzia matatizo yanayowakumba wanawake
A katika jamii
B wasio na upendo
C waliotelekezwa na waume zao
D walioachiwa watoto kuwalea peke yao
E wote wenye ndoa.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2592) Question Category: Ufahamu

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha andika ufupisho wa maneno 60 kuhusu habari hiyo.
Vijana popote duniani ni tegemeo la taifa. Kupuuza malezi ya vijana ni sawa na kupuuza uhai wa taifa. Leo hii tukitazama mwelekeo wa malezi ya watoto wetu, ipo hali ya kutatanisha sana. Sasa hivi malezi ya watoto hasa katika jumuiya yetu hapa Tanzania, yamekuwa na ugumu wa pekee. Baadhi ya vijana wetu wamejiingiza katika mambo ya aibu, mfano ulevi, uvutaji bangi, mambo ya ngono na vitendo vingine viovu. Sasa hivi baadhi yao hawana aibu tena na wanayumba maishani. Wengine wanapenda maisha ya starehe, njia za kujipatia mali haraka haraka na mengine mengi ya kusikitisha.
Tukumbuke kwamba hawa ndio wataiongoza nchi wakati wazee wao watakapomaliza muda wao wa kuishi hapa duniani. Lakini hebu tujiulize swali moja. Ni nani alaumiwe? Je tuwalaumu watoto? Tuwalaumu wazazi au nani?
Mambo ya burudani yalikuwepo tangu zamani lakini yalikuwa na mipaka yake. Mathalani ilikuwa ni mwiko kwa vijana wa kike kutembea peke yao, walitembea katika vikundi.
Tendo la kuzaa nje ya ndoa lilikuwa likilaumiwa vikali na ilikuwa ni aibu kwa binti yeyote
kukumbwa na balaa kama hilo.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2593) Question Category: Ufahamu

Soma habari ifuatayo kwa makini na kisha jibu maswali yanayofuata:
Wimbi la kusakama wahamiaji kutoka nchi jirani, hasa vijana wenye kazi, limeshika kasi katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini. Watu arobaini wameripotiwa kuuawa hadi sasa, mamia wamejeruhiwa, baadhi wakiwa wamechomwa moto. Vijana wenye mapanga, visu, nondo, nyundo na mishale wanawasaka mahamiaji majumbani, ofisini na mitaani.
Ghasia hizo zinatokana na vijana wa Afrika kusini kudai kwamba wanakosa ajira kwa sababu nafasi zao zinachukuliwa na wageni na wao kubaki wanazurura mitaani bila ya kazi. Wimbi hilo la vurugu na mauaji limeiharibia sifa Afrika Kusini nchi ambayo ilifikia hapo ilipo kwa msaada mkubwa wa hali na mali wa nchi za kusini mwa Afrika. Watu wa Afrika Kusini wamesahau kwamba wakati wa utawala wa makaburu, nchi jirani ziliwapokea maelfu kwa maelfu ya vijana na wazee wa Afrika Kusini kuwapa hifadhi pamoja na kusaidia mikakati ya mapambano dhidi ya makaburu. Pia vijana wa nchi hizo walikosa nafasi za masomo ya juu kutokana na wakimbizi wa Afrika Kusini kupewa upendeleo katika shule za sekondari na vyuo vikuu vya nchi hizo. Lakini leo hii watu wa nchi hizi wanaonekana si lolote si chochote nchini Afrika ya Kusini.
Hivi sasa vijana wengi wamekosa ajira katika nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Malawi na hata
Tanzania kwa vile makampuni ya Afrika ya Kusini yamechukua makampuni makubwa ya nchi hizo kama vile viwanda vya bia, mabenki na huajiri watu kutoka Afrika Kusini kufanya kazi huko. Suala hilo limehamasisha kukimbilia Afrika Kusini kwa vijana wengi ili kupata ajira.
Sasa njia pekee iliyobaki kwa vijana wa nchi jirani wasiokuwa na kazi ni kuzifuata ajira hizo Afrika Kusini. Wageni, hasa kutoka nchi za Afrika, wamekuwa wakikutana na vikwazo vya kupata vibali vya kufanya kazi, lakini wamekuwa wakitumia njia za panya kupata ajira. Vijana wengi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikosa ajira kutokana na elimu ndogo au maambukizi ya virusi vya UKIMWI yaliyozagaa nchini humu ukilinganisha na nchi jirani.
Takwimu za serikali, kwa mfano, zinaonesha zaidi ya asilimia thelathini (30%) ya wafanyakazi wa kwenye bandari ya mji wa Durban na maeneo ya ukanda wa Pwani, wanaishi na virusi vya UKIMWI na makampuni ya maeneo hayo yamekuwa yakibagua katika ajira maana uwezo wa watu hao kufanya kazi za sulubu ni mdogo kwa sababu ya UKIMWI.
Kwa ujumla ghasia zimezusha wasiwasi mkubwa kwa Afrika Kusini, nchi ambayo inakabiliwa na maandalizi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya fainali za Kombe la Dunia kwa mchezo wa soka mwaka 2010. Inatarajiwa kuvutia wageni wapatao nusu milioni. Wasiwasi unakuja kwa vile kiasi kikubwa cha fedha kimetumika katika maandalizi na faida yake inatarajiwa kupatikana wakati wa mashindano hayo. Hivyo vitendo vya mauaji vinatia doa. Upo uwezekano wa kukosa nafasi hiyo kutokana na kuhofia usalama na amani kwa wanamichezo.

Maswali
(a) Kichwa cha habari hii kinachofaa ni kipi?
(b) Vijana wengi kusini mwa Afrika wamemiminika Afrika Kusini ili wapate ajira. Eleza mambo
mawili (2) yaliyosababisha vijana hao wapate ajira Afrika ya Kusini.
(c) Ungeishauri nini serikali ya Afrika ya Kusini?
(d) Makampuni yanahofia kuwaajiri vijana wa Afrika Kusini. Ipi sababu kubwa ya hofu hiyo?

Answer / Solution

UNSOLVED

(2594) Question Category: Ufahamu

Soma habari ifuatayo kwa makini na kisha jibu maswali yanayofuata:
Wimbi la kusakama wahamiaji kutoka nchi jirani, hasa vijana wenye kazi, limeshika kasi katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini. Watu arobaini wameripotiwa kuuawa hadi sasa, mamia wamejeruhiwa, baadhi wakiwa wamechomwa moto. Vijana wenye mapanga, visu, nondo, nyundo na mishale wanawasaka mahamiaji majumbani, ofisini na mitaani.
Ghasia hizo zinatokana na vijana wa Afrika kusini kudai kwamba wanakosa ajira kwa sababu nafasi zao zinachukuliwa na wageni na wao kubaki wanazurura mitaani bila ya kazi. Wimbi hilo la vurugu na mauaji limeiharibia sifa Afrika Kusini nchi ambayo ilifikia hapo ilipo kwa msaada mkubwa wa hali na mali wa nchi za kusini mwa Afrika. Watu wa Afrika Kusini wamesahau kwamba wakati wa utawala wa makaburu, nchi jirani ziliwapokea maelfu kwa maelfu ya vijana na wazee wa Afrika Kusini kuwapa hifadhi pamoja na kusaidia mikakati ya mapambano dhidi ya makaburu. Pia vijana wa nchi hizo walikosa nafasi za masomo ya juu kutokana na wakimbizi wa Afrika Kusini kupewa upendeleo katika shule za sekondari na vyuo vikuu vya nchi hizo. Lakini leo hii watu wa nchi hizi wanaonekana si lolote si chochote nchini Afrika ya Kusini.
Hivi sasa vijana wengi wamekosa ajira katika nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Malawi na hata
Tanzania kwa vile makampuni ya Afrika ya Kusini yamechukua makampuni makubwa ya nchi hizo kama vile viwanda vya bia, mabenki na huajiri watu kutoka Afrika Kusini kufanya kazi huko. Suala hilo limehamasisha kukimbilia Afrika Kusini kwa vijana wengi ili kupata ajira.
Sasa njia pekee iliyobaki kwa vijana wa nchi jirani wasiokuwa na kazi ni kuzifuata ajira hizo Afrika Kusini. Wageni, hasa kutoka nchi za Afrika, wamekuwa wakikutana na vikwazo vya kupata vibali vya kufanya kazi, lakini wamekuwa wakitumia njia za panya kupata ajira. Vijana wengi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikosa ajira kutokana na elimu ndogo au maambukizi ya virusi vya UKIMWI yaliyozagaa nchini humu ukilinganisha na nchi jirani.
Takwimu za serikali, kwa mfano, zinaonesha zaidi ya asilimia thelathini (30%) ya wafanyakazi wa kwenye bandari ya mji wa Durban na maeneo ya ukanda wa Pwani, wanaishi na virusi vya UKIMWI na makampuni ya maeneo hayo yamekuwa yakibagua katika ajira maana uwezo wa watu hao kufanya kazi za sulubu ni mdogo kwa sababu ya UKIMWI.
Kwa ujumla ghasia zimezusha wasiwasi mkubwa kwa Afrika Kusini, nchi ambayo inakabiliwa na maandalizi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya fainali za Kombe la Dunia kwa mchezo wa soka mwaka 2010. Inatarajiwa kuvutia wageni wapatao nusu milioni. Wasiwasi unakuja kwa vile kiasi kikubwa cha fedha kimetumika katika maandalizi na faida yake inatarajiwa kupatikana wakati wa mashindano hayo. Hivyo vitendo vya mauaji vinatia doa. Upo uwezekano wa kukosa nafasi hiyo kutokana na kuhofia usalama na amani kwa wanamichezo.

Swali:

Andika ufupisho wa aya mbili za mwisho za habari uliyoisoma kwa maneno hamsini (50) .

Answer / Solution

UNSOLVED

(2595) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yatakayofuata:
Kwa neno zima uzalendo ni mapenzi ya nchi. Mapenzi haya hayafanyiki kwa njia za kubuniwa na watu lakini yamekwishatangulia kuwa katika mioyo yetu. Uzalendo ni tabia ya maumbile, nasi tunayo toka wakati wa kuzaliwa. Tunafikiri habari za nchi yetu kama tufikiriavyo habari za baba na mama zetu; kwa hivi kila mtu anajali sana mahali alipozaliwa.
Baadhi ya watu hawakubali nao wako tayari siku zote kupinga pishi ya hoja zako kwa ukufi wa hoja zao. Wao hufikiri kwamba uzalendo ni maono ya ushupavu na dalili ya uchache wa ustaarabu wa moyo. Kwao uzalendo ni imani ya kishenzi, kwa sababu hutenga kando nchi nyingine.
Wanadai kwamba mtu ni lazima apende ulimwengu mzima na watu wa ulimwengu hufanya kila mtu kuwa raia wa dunia si wa mahali pake padogo pajulikanapo kama nchi yake. Lazima niseme kweli kwamba wazo la udugu wa ulimwengu ni bora kwa makisio lakini kwa matumizi haliwezekani. Bora katika watu ni yule apendaye nchi yake kwanza. Kuna mashaka makubwa kama mtu anaweza kuamini katika mapenzi ya udugu wa ulimwengu bila kupenda nchi yake ikiwa hivyo, uzalendo huthibitisha ubora wa kupenda sehemu ya ulimwengu ambayo ndani yake tumezaliwa.
Mapenzi ya mtu kwa nchi yake hayaoneshi chuki ya nchi nyingine za ulimwengu. Uzalendo wa uwongo ndiyo utufanyao kuchukia nchi nyingine. Aidha, lazima tupende nchi zetu kwa sababu ya nchi zenyewe. Pasiwe na kusudi baya au la choyo nyuma yake. Kuna uzalendo wa uwongo vilevile ambao ni hila tufanyayo kwa makusudi yetu wenyewe ya choyo kwa sababu ya nia mbaya za kujitajirisha. Uzalendo wa kweli hutokana na mapenzi yasiyo na choyo ya nchi zetu na heshima yetu ya historia na malezi. Uzalendo usitufanye kujiona kwamba sisi ni watu azizi ulimwenguni na makabila mengine yote si kitu.
Mapenzi ya nchi zetu huonekana kama maono bora lakini hayana maana kama hayachukuani na matendo. Uzalendo wa matendo tu ndio wenye thamani nchini iwapo katika hatari ya shambulio la adui. Mapenzi ya mtu kwa nchi yasiyo ya matendo yanaweza kuwa mema katika nyakati za amani, lakini katika nyakati za vita uzalendo huthibitisha unyofu wake katika kitali. Uzalendo hutaka sadaka za maisha, jamaa, mali na kila kitu cha mtu. Watu wanaotoa sadaka za maisha yao kwa sababu ya nchi zao ni mashahidi.

Maswali
(a) Mwandishi ana misimamo gani kuhusu uzalendo?
(b) Mwandishi anatoa angalizo gani kuhusu uzalendo?
(c) “Kupinga pishi ya hoja zako kwa ukufu wa hoja zao.” Usemi huu una maana gani kulingana na
habari uliyoisoma?
(d) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu cha habari ulichosoma.

Answer / Solution

UNSOLVED

View All Topics
News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02

questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29

questions

2024-03-19: questions

Questions Uploaded on 2024-03-19

Dismissible in 10 seconds