Ufahamu questions | form four Kiswahili

(2606) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Ustaarabu ni jambo jema ambalo hupendwa na kila jamii yenye utashi hapa duniani. Kila jamii yenye ustaarabu mambo yake huendeshwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazoeleweka.
Maamuzi na mafanikio mbalimbali miongoni mwa wanajamii hutolewa bila hamaki wala
kukurupuka. Kanuni na taratibu hizo huiongoza jamii kufikia upeo wake kimaendeleo kuanzia ngazi za chini kabisa ambayo ni familia mpaka ngazi ya juu kabisa ambayo ni taifa. Taratibu na kanuni hizo huwekwa katika chombo kimoja maalumu kinachoitwa katiba.
Katiba ni jumla ya sheria, kanuni na taratibu fulani zilizokubaliwa kuwekwa na jamii au taifa fulani kama dira ya maisha ya kila siku ya jamii au taifa hilo. Taifa bila katiba ni sawa na behewa la garimoshi bila injini. Hivyo katiba ina umuhimu wa kipekee katika taifa lolote lile.
Katika nchi zenye utamaduni wa kidemokrasia, katiba huundwa kutokana na maoni ya wananchi wake kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali. Aghalbu, maoni na mawazo yaliyotolewa na wananchi huwa ni chimbuko la katiba hiyo. Wananchi hujiona ni sehemu ya utawala. Kwa upande wa pili wa sarafu, nchi zenye utaratibu wa kiimla , katiba hutayarishwa na watawala kwa maslahi yao binafsi. Katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala. Maoni na mawazo ya wananchi hayazingatiwi katika kuunda katiba.
Umuhimu wa katiba huonekana na kujidhihirisha waziwazi katika maisha ya kila siku ya nchi yoyote ile. Kwanza, katiba huelekeza wajibu wa ila mwanajamii kwa taifa lake na wajibu wa viongozi walio madarakani kwa wananchi au raia. Pili, katiba huonesha na kuainisha haki ambazo kila raia anastahili kupata na pia taratibu za kufuata katia kudai au dupewa haki hizo.

Mbali na hayo, katiba hutoa utaratibu wa jinsi ya kuwapata viongozi wetu katika ngazi mabalimbali za kisiasa na kijamii. Pia uhuru wa mtu binafsi hulindwa na katiba. Hivyo, katika nchi ambayo ina katiba inayokidhi matarajio ya wananchi wote mambo huwa mazuri na kamwe chombo hakiwezi kwenda mrama .
Aidha, wananchi hawana budi kuelewa maana ya katiba ili waweze kutoa maoni na mapendekezo ya kuunda katiba mpya au kuimarisha iliyopo. Ni muhali kwa mtu asiyejua maana ya katiba kutoa maoni kuhusu katiba. Wananchi hupaswa kuelimishwa kupita semina, warsha na makongamano mbalimbali ili kujua katiba zao na kutoa maoni kuhusu uundaji wa katibu mpya.
Hata hivyo, wananchi wengi hasa vijana hawajitumi katika kuzijua katiba za nchi zao au kutoa maoni ya uundaji wa katiba mpya. Athari zake ni kutojua haki zao za msingi na kuburutwa kama mkokoteni na watawala katika mambo mbalimbali. Vilevile hulalamikia mambo ambayo hawakuchangia mawazo.
Hivyo basi, ni vizuri kwa wananchi kutambua, kuthamini na kuheshimu uwepo wa katiba kama kiongozi kizuri katika kuonesha njia muafaka ya kujiletea maendeleo kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa nchi husika.

Maswali
(a) Toa maana ya maneno yote yaliyokolezwa wino kama yalivyotumika katika habari uliyosoma.
(b) Kwa mujibu wa habari uliyosoma, taja mambo mazuri mawili yatokanayo na uwepo wa katiba katika nchi.
(c) Kwanini mwandishi anasema katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala?
(d) Je, ni hofu gani aliyonayo mwandishi dhidi ya vijana kuhusu katiba?
(e) Andika kichwa cha habari uliyosoma kisichozidi maneno matano (5).

Answer / Solution

UNSOLVED

(2607) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Ustaarabu ni jambo jema ambalo hupendwa na kila jamii yenye utashi hapa duniani. Kila jamii yenye ustaarabu mambo yake huendeshwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazoeleweka.
Maamuzi na mafanikio mbalimbali miongoni mwa wanajamii hutolewa bila hamaki wala
kukurupuka. Kanuni na taratibu hizo huiongoza jamii kufikia upeo wake kimaendeleo kuanzia ngazi za chini kabisa ambayo ni familia mpaka ngazi ya juu kabisa ambayo ni taifa. Taratibu na kanuni hizo huwekwa katika chombo kimoja maalumu kinachoitwa katiba.
Katiba ni jumla ya sheria, kanuni na taratibu fulani zilizokubaliwa kuwekwa na jamii au taifa fulani kama dira ya maisha ya kila siku ya jamii au taifa hilo. Taifa bila katiba ni sawa na behewa la garimoshi bila injini. Hivyo katiba ina umuhimu wa kipekee katika taifa lolote lile.
Katika nchi zenye utamaduni wa kidemokrasia, katiba huundwa kutokana na maoni ya wananchi wake kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali. Aghalbu, maoni na mawazo yaliyotolewa na wananchi huwa ni chimbuko la katiba hiyo. Wananchi hujiona ni sehemu ya utawala. Kwa upande wa pili wa sarafu, nchi zenye utaratibu wa kiimla , katiba hutayarishwa na watawala kwa maslahi yao binafsi. Katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala. Maoni na mawazo ya wananchi hayazingatiwi katika kuunda katiba.
Umuhimu wa katiba huonekana na kujidhihirisha waziwazi katika maisha ya kila siku ya nchi yoyote ile. Kwanza, katiba huelekeza wajibu wa ila mwanajamii kwa taifa lake na wajibu wa viongozi walio madarakani kwa wananchi au raia. Pili, katiba huonesha na kuainisha haki ambazo kila raia anastahili kupata na pia taratibu za kufuata katia kudai au dupewa haki hizo.

Mbali na hayo, katiba hutoa utaratibu wa jinsi ya kuwapata viongozi wetu katika ngazi mabalimbali za kisiasa na kijamii. Pia uhuru wa mtu binafsi hulindwa na katiba. Hivyo, katika nchi ambayo ina katiba inayokidhi matarajio ya wananchi wote mambo huwa mazuri na kamwe chombo hakiwezi kwenda mrama .
Aidha, wananchi hawana budi kuelewa maana ya katiba ili waweze kutoa maoni na mapendekezo ya kuunda katiba mpya au kuimarisha iliyopo. Ni muhali kwa mtu asiyejua maana ya katiba kutoa maoni kuhusu katiba. Wananchi hupaswa kuelimishwa kupita semina, warsha na makongamano mbalimbali ili kujua katiba zao na kutoa maoni kuhusu uundaji wa katibu mpya.
Hata hivyo, wananchi wengi hasa vijana hawajitumi katika kuzijua katiba za nchi zao au kutoa maoni ya uundaji wa katiba mpya. Athari zake ni kutojua haki zao za msingi na kuburutwa kama mkokoteni na watawala katika mambo mbalimbali. Vilevile hulalamikia mambo ambayo hawakuchangia mawazo.
Hivyo basi, ni vizuri kwa wananchi kutambua, kuthamini na kuheshimu uwepo wa katiba kama kiongozi kizuri katika kuonesha njia muafaka ya kujiletea maendeleo kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa nchi husika.

Swali:

Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua mia moja (100).

Answer / Solution

UNSOLVED

(2608) Question Category: Ufahamu

Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:
Ima mwana wende kasi, ima usirudi nyuma
Ima ukwepe sabasi, ima ukipite kima
Ima ujivike lasi, ima ndiyo taadhima
Ima mwanakwetu ima, dunia ni sarakasi.

Ima kasema mkwasi , ima uende kulima
Ima njaa sikughasi, ima mgongo inama
Ima wepuke uasi, ima upate usalama
Ima mwanakwetu ima, ima ndipo utapasi.

Ima ndipo utapasi , ima mwanakwetu ima
Ima ujiunge nasi, ima tuujenge umma
Ima usile najisi, ima ule cha kuchuma
Ima mwanakwetu ima, ima emaye hakosi.

Ima emaya hakosi, ima jikalifu ima
Ima upweke tatasi, ima wewe na Mwajuma
Ima yoyomea kusi, ima usiuye nyuma
Ima wa ima faima, ima upate fulusi.

Ima wmanakwetu basi, ima usende kinyuma
Ima kazi ni libasi , ima inama kulima
Ima wacha udadisi, ima nakwambia ima
Ima usikae ima, kama kuishi wahisi.

Maswali
(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi ulilolisoma:
(i) Mkwasi
(ii) Utapasi
(iii) Jikalifu
(iv) Libasi
(b) Kwa kutumia sentensi tatu (3), fafanua ujumbe wa mwandishi katika shairi hili.
(c) Msanii ana maana gani anaposema “Ima mwanakwetu ima, dunia ni sarakasi.”

Answer / Solution

UNSOLVED

(2609) Question Category: Ufahamu

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha fupisha habari hii kwa maneno hamsini (50).
Kijana anahitaji kuwa na rafiki ili aweze kuondokana na ukiwa pia ili aweze kupata faraja. Aidha hayo yatajitokeza kwa sababu atafahamiana na marafiki hao, vilevile atazoeana nao hasa kwa kupitia maongezi. Kijana huweza kupata marafiki popote, kwa mfano miongoni mwa majirani zake, shuleni, kazini, sehemu za ibada na hata awapo safarini. Lakini kijana anapaswa kuwa mwangalifu katika kuchagua marafiki.
Katika makuzi yake kijana huwa karibu sana na rafiki zake ambao kwa kiasi kikubwa huwa na nguvu na ni rahisi kwa rafiki kuambukizana tabia ambazo zaweza kuwa nzuri au mbaya. Kwa hiyo ni jukumu la wazazi kumwelekeza kijana na kumshauri kuhusu ni yupi hasa rafiki mwema. Ni heri kukosa rafiki kuliko kuwa na rafiki mlevi, mwongo, mwizi, mvivu, mvuta bangi au mtumiaji wa dawa za kulevya. Rafiki mzuri ni yule mwenye tabia njema na busara ambaye hutoa ushauri mzuri unaoweza kumsaidia mtu kupata mafanikio katika maisha.

Answer / Solution

UNSOLVED

(4962) Question Category: Ufahamu

Soma​ ​ kifungu​ ​ cha​ ​ habari​ ​ kifuatacho​ ​ kisha​ ​ jibu​ ​ maswali​ ​ yanayofuata.

Suala la kuwapenda na kuwajali watoto ni muhimu sana kaitka jamii. Leo hii suala la kuwaonesha watoto mapenzi limekuwa na jambo la ziada kwa watu na familia nyingi. Kuna mambo mengine mengi​ ​ maishani​ ​ mwetu​ ​ ambayo​ ​ watu​ ​ wengi​ ​ huyaona​ ​ kuwa​ ​ muhimu​ ​ zaidi​ ​ badala​ ​ ya​ ​ watoto.

Kuna vitendo vingi vya ukatili ambavyo watoto hutendewa. Hivi majuzi kumekuwa na visa vya watoto wengi wachanga kutupwa majalalani. Viumbe hawa walipokatiziwa uhai, maiti zao zilitupwa kama takataka na hiyo ni miili ambayo ilipatikana jalalani. Lakini wengi wanajiuliza kuna maelfu mangapi ya miili mingine kama hiyo inayotupwa? Hili lilikuwa tone dogo la bahari ya dhambi ambazo sote tunaogelea ndani. Ni vema kila mtu kwa nafasi yake katika jamii, kuwaokoa watoto
wetu,​ ​ ili​ ​ tusije​ ​ tukawalilia​ ​ baadaye.

Mambo kama haya ni mazao ya mimiea yetu ambayo tuliipanda sisi ambao hutachelewi kujiita watu walio huru, walio na maendeleo na wa kisasa. Tumekuwa watu wa kupuuza mambo ya kimapokeo ya kuzingatia utu na kuficha aibu. Aghalabu tumejitia usasa kwa kutazama filamu na video zisizokuwa na maadili, kusikiliza muziki wenye maneno yasiyokuwa na maadili. Tunapoona watoto wetu wakitembea nusu uchi, hatushughuliki hata kidogo kuwakanya na matokeo yake ni hapo
tulipofikia sasa. Kama ni kosa, sisi sote tumehusika kwa njia moja au nyingine. Ni vizuri tuelewe kuwa​ ​ sisi​ ​ ni​ ​ watunzaji​ ​ na​ ​ walezi​ ​ wa​ ​ ndugu​ ​ zetu​ ​ kwa​ ​ kila​ ​ njia.

Tutawaokoa watoto kwa kukataa mambo yote yanayowanyanyasa. Lazima tuwaoneshe watoto mapenzi. Mapenzi si chakula, mavazi na makazi tu. Mapenzi si kuwaachia vijana uhuru watende wapendavyo. Mapenzi sio kuwanunulia vitu vya bei ghali au kuacha kuwakemea wanapokosa mwelekeo. Mapenzi kwa watoto ni kuwaheshimu na kuwatendea kama binadamu yeyote. Lazima mzazi akumbuke kwamba mtoto hujifunza kutoka kwake. Mtoto atamtendea mzazi jinsi alivyotendwa. Aidha, jinsi mzazi anavyomtendea mtoto wake ndivyo atakavyowatendea watoto
wake​ ​ na​ ​ wale​ ​ wote​ ​ ambao​ ​ atapata​ ​ kuhusiana​ ​ nao​ ​ kwa​ ​ njia​ ​ moja​ ​ au​ ​ nyingine.

Wazazi ni lazima wawaokoe watoto wao katika viwango vyote vya ukuaji, kusiwe na mwanya baina ya mzazi na mtoto. Watoto waweze kuwaambia wazazi yote yanayowahangaisha mioyoni mwao, na hali hii itawapa wazazi fursa ya kuwasaidia. Mtoto anapokosa wazazi wawe tayari kumwonesha kosa​ ​ lake​ ​ na​ ​ kumwadhibu​ ​ kwa​ ​ mapenzi.

Mtoto mwingine yeyote akipotoka wazazi wawe tayari kumkosoa na kuwaarifu wazazi wake.Tuache ubinafsi wetu, tukumbuke kuwa mwana wa mwenzio ni wako pia. Ni jambo la busara kuhaikikisha​ ​ kwamba​ ​ kama​ ​ wazazi,​ ​ tuzingatie​ ​ haki​ ​ zote​ ​ za​ ​ watoto.

Maswali
1. (a) Pendekeza​ ​ kichwa​ ​ kinachofaa​ ​ kwa​ ​ habari​ ​ hii​ ​ kisichozidi​ ​ maneno​ ​ manne.
(b) Fafanua​ ​ chanzo​ ​ cha​ ​ mienendo​ ​ isiyofaa​ ​ kwa​ ​ vijana​ ​ kama​ ​ kilivyoelezwa​ ​ na​ ​ mwandishi.
(c) Kwa​ ​ nini​ ​ mwandishi​ ​ anasema​ ​ sisi​ ​ sote​ ​ tumehusika​ ​ na​ ​ mienendo​ ​ mibaya​ ​ ya​ ​ watoto​ ​ wetu?
(d) Mwandishi​ ​ anatoa​ ​ msimamo​ ​ gani​ ​ kwa​ ​ wazazi​ ​ kuhusu​ ​ suala​ ​ la​ ​ mapenzi​ ​ katika​ ​ malezi​ ​ ya​ ​ watoto wetu.
(e) “Mtoto​ ​ wa​ ​ mwenzetu​ ​ akipotoka,​ ​ pia​ ​ tuwe​ ​ tayari​ ​ kumkosoa.”​ ​ Unafikiri​ ​ kwa​ ​ mazingira​ ​ ya​ ​ sasa inawezekana?​ ​ Toa​ ​ maoni​ ​ yako.

2. Fupisha​ ​ habari​ ​ uliyosoma​ ​ kwa​ ​ maneno​ ​ mia​ ​ moja​ ​ (100).

Answer / Solution

UNSOLVED

View All Topics
News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02

questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29

questions

2024-03-19: questions

Questions Uploaded on 2024-03-19

Dismissible in 10 seconds