Ufahamu questions | form four Kiswahili

(2596) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yatakayofuata:
Kwa neno zima uzalendo ni mapenzi ya nchi. Mapenzi haya hayafanyiki kwa njia za kubuniwa na watu lakini yamekwishatangulia kuwa katika mioyo yetu. Uzalendo ni tabia ya maumbile, nasi tunayo toka wakati wa kuzaliwa. Tunafikiri habari za nchi yetu kama tufikiriavyo habari za baba na mama zetu; kwa hivi kila mtu anajali sana mahali alipozaliwa.
Baadhi ya watu hawakubali nao wako tayari siku zote kupinga pishi ya hoja zako kwa ukufi wa hoja zao. Wao hufikiri kwamba uzalendo ni maono ya ushupavu na dalili ya uchache wa ustaarabu wa moyo. Kwao uzalendo ni imani ya kishenzi, kwa sababu hutenga kando nchi nyingine.
Wanadai kwamba mtu ni lazima apende ulimwengu mzima na watu wa ulimwengu hufanya kila mtu kuwa raia wa dunia si wa mahali pake padogo pajulikanapo kama nchi yake. Lazima niseme kweli kwamba wazo la udugu wa ulimwengu ni bora kwa makisio lakini kwa matumizi haliwezekani. Bora katika watu ni yule apendaye nchi yake kwanza. Kuna mashaka makubwa kama mtu anaweza kuamini katika mapenzi ya udugu wa ulimwengu bila kupenda nchi yake ikiwa hivyo, uzalendo huthibitisha ubora wa kupenda sehemu ya ulimwengu ambayo ndani yake tumezaliwa.
Mapenzi ya mtu kwa nchi yake hayaoneshi chuki ya nchi nyingine za ulimwengu. Uzalendo wa uwongo ndiyo utufanyao kuchukia nchi nyingine. Aidha, lazima tupende nchi zetu kwa sababu ya nchi zenyewe. Pasiwe na kusudi baya au la choyo nyuma yake. Kuna uzalendo wa uwongo vilevile ambao ni hila tufanyayo kwa makusudi yetu wenyewe ya choyo kwa sababu ya nia mbaya za kujitajirisha. Uzalendo wa kweli hutokana na mapenzi yasiyo na choyo ya nchi zetu na heshima yetu ya historia na malezi. Uzalendo usitufanye kujiona kwamba sisi ni watu azizi ulimwenguni na makabila mengine yote si kitu.
Mapenzi ya nchi zetu huonekana kama maono bora lakini hayana maana kama hayachukuani na matendo. Uzalendo wa matendo tu ndio wenye thamani nchini iwapo katika hatari ya shambulio la adui. Mapenzi ya mtu kwa nchi yasiyo ya matendo yanaweza kuwa mema katika nyakati za amani, lakini katika nyakati za vita uzalendo huthibitisha unyofu wake katika kitali. Uzalendo hutaka sadaka za maisha, jamaa, mali na kila kitu cha mtu. Watu wanaotoa sadaka za maisha yao kwa sababu ya nchi zao ni mashahidi.

Swali:

Andika muhtasari wa aya mbili (2) za mwisho za habari uliyoisoma kwa maneno yasiyozidi sitini
(60).

Answer / Solution

UNSOLVED

(2597) Question Category: Ufahamu

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yatakayofuata:
Sikukuu ya kusherehekea uvunaji wa viazi vipya ilikuwa inakaribia na Umuofia ilikuwa katika hali ya matayarisho. Hii ilikuwa ndiyo siku ambayo watu walitoa kafara kwa Ani, Mungu wa rutuba ya ardhi na mwamuzi wa mwenendo na uadilifu wa watu wote. Alikuwa Mungu aliyehusika sana na maisha ya watu na mababu wa Umuofia waliozikwa katika ardhi yake.
Kwa sababu hii, sikukuu ilifanywa kila mwaka kabla mavuno hayajaanza. Hakuna mtu ambaye angeweza kula viazi vipya kabla havijatolewa sadaka kwa Ani au Mahoka wa mababu wa Umuofia. Watu wote waliifurahia siku hii na kuingoja kwa u chu mkubwa kwa sababu yalikaribia majira ya vyakula maridhawa mwaka mpya. Watu wote waliokuwa na viazi vya mwaka uliopita ilibidi wavitupilie mbali kabla ya sikukuu hii haijaanza. Mwaka mpya ulitakiwa kuanzwa na vyakula vipya vilivyo vinono. Haikuwa heshima wala jambo la faraja kuendelea na vile vilivyokauka kutoka mwaka jana. Hata vyombo vya kupikia na vya kulia vilioshwa barabara. Kinu kile ambamo viazi vipya vilitwangwa kililazimu kusuguliwa sana.
Sikukuu ya viazi lilikuwa tukio la nderemo Umuofia nzima. Yeyote aliyekuwa na m kono wenye nguvu kama wazee wasemavyo alitegemea kualika wageni wengi kutoka karibu na mbali. Okonkwo aliwaalika ndugu wa wake zake na kwa sababu alikuwa na wake watatu, wageni hao walikuwa wengi wa kutosha.
Lakini ingawa hivyo, Okonkwo hakuwa mtu wa kufurahia sikukuu za aina yoyote. Ni kweli kwamba yeye aliweza kula sana, hata alipokunywa tembo alimaliza vibuyu vikubwa lakini kule kukaa bure bila kazi ndiko kulikomfanya asiwe na furaha. Furaha yake ilikuwa katika kazi ya shamba.
Sasa sikukuu ilikuwa imekaribia na wake zake Okonkwo walisugua kuta za vibanda vyao kwa udongo wa aina mbalimbali. Wao wenyewe walijipamba kwa kuchorachora matumbo yao na migongo. Wageni wengi walikuwa wamealikwa hata Ikemefuna alikuwa katika s hamrashamra hiyo. Kwao pia kulikuwa na sikukuu kama hii lakini hapa ilionekana kubwa na ya kufana zaidi. Na kwao sasa kilikuwa kitu kilichoanza kupotea katika dunia ya kumbukumbu yake.

Maswali
(a) Eleza sababu mbili (2) zilizowafanya wananchi wa Umuofia waisubiri kwa uchu mkubwa siku iliyoelezewa kwenye kifungu cha habari.
(b) Kwa mujibu wa kifungu cha habari, eleza sifa moja (1) iliyomtofautisha Okonkwo na watu wengine wa Umuofia.
(c) Eleza maana ya maneno au kifungu cha maneno kilichokolezwa wino.
(d) Unafikiri ni sababu ipi kubwa iliyosababisha kutupwa kwa viazi vyote vya zamani na vyombo vyote kuoshwa?
(e) Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano (5) kinachofaa kwa habari uliyosoma.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2598) Question Category: Ufahamu

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha andika ufupisho wa maneno sitini (60) kuhusu habari hiyo. Kwa miaka mingi baadhi ya mila na desturi zetu zimetufunga hadi kutufikisha mahali ambapo imekuwa ni vigumu kwetu kubaini ukweli kuhusu mambo muhimu yanayotuzunguka, yakiwa ni yale yanayohusu sisi na miili yetu na yale yaliyonje ya miili hii. Kwa mfamo hadi leo kuna watoto wa umri mkubwa kufikia miaka saba ambao hawajui majina ya baba au mama zao. Lakini pia kuna vijana wa umri wa kuvunja ungo au balehe ambao hawajui ni kwa vipi mtoto anapatikana hasa maeneo ya vijijini. Kuna watu wazima ambao hadi leo mjadala kuhusu kifo ukiingizwa kenye mazungumzo huwa hawako tayari kusikiliza wakiamini kuwa huo ni mwiko na uchoro mkubwa. Hali hii kwa sehemu kubwa inatokana na desturi na mila zetu ambazo zimepogoka na zinahitaji kutazamwa upya kama zina faida kwa jamii. Baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakichukuliwa kama mwiko mkubwa kuyajadili hadharani au hata kati ya watu zaidi ya mmoja ni yale yanayohusu mbegu za kiume, yai la mwanamke na upatikanaji wa mimba.
Siyo jambo la siri kwamba mada zenye kuhusu mambo haya ni nadra sana kujadiliwa katika jamii zetu na wengi ni maamuma kabisa kuhusiana na masuala haya. Inawezekana ikawashangaza wengi pale mtu atakaposema kuwa mwanamume anaweza kumpa mimba mwanamke bila mwanamume huyo kukutana kimwili na mwanamke anayehusika.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2599) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Misitu ya nchi ni mingi sana hata wakati mwingine tunadanganyika kuwa haitakwisha kamwe.

Tunaamini kwamba tunaweza kuendelea kuitumia miti yake na kuikata kwa ajili ya kupata mashamba na malisho ya wanyama wetu bila kujishughulisha kupanda au kuhifadhi mingine kwa ajili ya siku za mbele. Fikiria tulivyo na mawazo potofu. Fikira mbaya kama hizo wanazo watu wengi nchini mwetu. Kwa hiyo imenilazimu kuwaonesheni kuwa misitu ni lazima ilindwe na haitalindwa kwa manufaa ya kizazi chetu cha sasa tu, bali pia kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.
Basi mjue kuwa kama misitu yote itakatwa patakuwa na upungufu mkubwa wa mbao na pia upungufu wa maji ambao ni mbaya zaidi. Ubaya kama huu hautakiwi utokee katika Taifa letu linalosonga mbele. Hatuwezi kuruhusu uharibifu wa misitu yetu uendelee kufanyika kwa sababu unarudisha nyuma hali ya maisha yetu na unazuia ustawi wa nchi yetu. Hebu fikiria kwanza maisha yetu yatakuwaje iwapo miti itakosekana taabu
ya kupika, gharama ya kujenga kwa chuma, mawe au udongo ulaya badala ya miti. Gharama ya viti, vitanda na meza ikiwa vitatengenezwa kwa chuma tu. Halafu fikiria kama maji yote yakikauka, ninyi nyote mwajua shida zitakazotokea, kwa hiyo hatutaki kabisa shida kutokea.
Kwa nini tuwe na shida ya kukosa maji katika sehemu ambazo zina maji ya kutosha? Basi inatupasa kuona kwamba kuna ulazima wa kuhifadhi misitu kwa ajili ya matumizi ya leo na kesho. Bila shaka sasa utajiuliza mwenyewe. Je, siwezi kukata kabisa misitu ili niweze kulima? Jibu ni kwamba unaweza kabisa, lakini ni katika sehemu zile ambazo hazikuhifadhiwa. Tena ifahamike kwamba sehemu ambazo zimehifadhiwa ni chache sana ukilinganisha na mapori makubwa yaliyobaki wazi kwa ajili ya kilimo.
Sasa nataka kusisitiza hasa juu ya misitu iliyohifadhiwa. Hizi ndizo sehemu za misitu ambazo ni za lazima sana, na inatakiwa zihifadhiwe daima kwa matumizi ya faida ya Taifa. Misitu iliyohifadhiwa ni misitu inayotazamiwa kudumu daima nchini. Inatunzwa ili itumiwe kwa utaratibu ulio bora kwa kizazi hata kizazi. Kwa wakati ujao misitu hiyo itatoa mbao za kujenga nyumba, shule, hospitali na majengo mengine, pia kutengeneza viti, meza, makabati, milango, madirisha na masanduku. Hata sasa, mbao nyingi zitumikazo hutokana na miti iliyoota katika misitu iliyohifadhiwa. Lakini kwa sababu ardhi yenye misitu ya aina hiyo inahitajiwa sana kwa kilimo, itatubidi kuanza kuotesha misitu mipya kwa ajili ya mahitaji yetu. Basi ni lazima niwakumbushe wananchi kuwa miti iliyomo katika misitu iliyohifadhiwa haitatosha kufanyia kazi zetu zote ili kuinua maisha ya watu na kuinua
uchumi wa nchi. Misitu iliyohifadhiwa lazima iongezwe kwa kupanda miti mingine, kwa mfano hivi sasa Idara ya misitu inapanda miti kati ya eka elfu nne na tano kila mwaka na pia inaangalia miti ya asili katika sehemu kubwa kabisa ya nchi hii.

Maswali
(a) Kwa mujibu wa habari uliyosoma watu wengi hufikiria nini juu ya misitu?
(b) Mwandishi wa habari hii anasema ni jambo gani huleta uharibifu wa misitu?
(c) Mwandishi anashauri misitu ikatwe katika sehemu gani?
(d) Je, ni madhara gani yatatokea endapo misitu itatoweka kabisa?
(e) Je, ni sahihi kusema kuwa kwa vile kuna misitu iliyohifadhiwa hakuna haja ya kushughulika na kupanda miti nchini? Kwa nini?

Answer / Solution

UNSOLVED

(2600) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Misitu ya nchi ni mingi sana hata wakati mwingine tunadanganyika kuwa haitakwisha kamwe.

Tunaamini kwamba tunaweza kuendelea kuitumia miti yake na kuikata kwa ajili ya kupata mashamba na malisho ya wanyama wetu bila kujishughulisha kupanda au kuhifadhi mingine kwa ajili ya siku za mbele. Fikiria tulivyo na mawazo potofu. Fikira mbaya kama hizo wanazo watu wengi nchini mwetu. Kwa hiyo imenilazimu kuwaonesheni kuwa misitu ni lazima ilindwe na haitalindwa kwa manufaa ya kizazi chetu cha sasa tu, bali pia kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.
Basi mjue kuwa kama misitu yote itakatwa patakuwa na upungufu mkubwa wa mbao na pia upungufu wa maji ambao ni mbaya zaidi. Ubaya kama huu hautakiwi utokee katika Taifa letu linalosonga mbele. Hatuwezi kuruhusu uharibifu wa misitu yetu uendelee kufanyika kwa sababu unarudisha nyuma hali ya maisha yetu na unazuia ustawi wa nchi yetu. Hebu fikiria kwanza maisha yetu yatakuwaje iwapo miti itakosekana taabu
ya kupika, gharama ya kujenga kwa chuma, mawe au udongo ulaya badala ya miti. Gharama ya viti, vitanda na meza ikiwa vitatengenezwa kwa chuma tu. Halafu fikiria kama maji yote yakikauka, ninyi nyote mwajua shida zitakazotokea, kwa hiyo hatutaki kabisa shida kutokea.
Kwa nini tuwe na shida ya kukosa maji katika sehemu ambazo zina maji ya kutosha? Basi inatupasa kuona kwamba kuna ulazima wa kuhifadhi misitu kwa ajili ya matumizi ya leo na kesho. Bila shaka sasa utajiuliza mwenyewe. Je, siwezi kukata kabisa misitu ili niweze kulima? Jibu ni kwamba unaweza kabisa, lakini ni katika sehemu zile ambazo hazikuhifadhiwa. Tena ifahamike kwamba sehemu ambazo zimehifadhiwa ni chache sana ukilinganisha na mapori makubwa yaliyobaki wazi kwa ajili ya kilimo.
Sasa nataka kusisitiza hasa juu ya misitu iliyohifadhiwa. Hizi ndizo sehemu za misitu ambazo ni za lazima sana, na inatakiwa zihifadhiwe daima kwa matumizi ya faida ya Taifa. Misitu iliyohifadhiwa ni misitu inayotazamiwa kudumu daima nchini. Inatunzwa ili itumiwe kwa utaratibu ulio bora kwa kizazi hata kizazi. Kwa wakati ujao misitu hiyo itatoa mbao za kujenga nyumba, shule, hospitali na majengo mengine, pia kutengeneza viti, meza, makabati, milango, madirisha na masanduku. Hata sasa, mbao nyingi zitumikazo hutokana na miti iliyoota katika misitu iliyohifadhiwa. Lakini kwa sababu ardhi yenye misitu ya aina hiyo inahitajiwa sana kwa kilimo, itatubidi kuanza kuotesha misitu mipya kwa ajili ya mahitaji yetu. Basi ni lazima niwakumbushe wananchi kuwa miti iliyomo katika misitu iliyohifadhiwa haitatosha kufanyia kazi zetu zote ili kuinua maisha ya watu na kuinua
uchumi wa nchi. Misitu iliyohifadhiwa lazima iongezwe kwa kupanda miti mingine, kwa mfano hivi sasa Idara ya misitu inapanda miti kati ya eka elfu nne na tano kila mwaka na pia inaangalia miti ya asili katika sehemu kubwa kabisa ya nchi hii.

Swali:

Fupisha aya tatu (3) za mwisho za habari uliyosoma kwa maneno themanini (80).

Answer / Solution

UNSOLVED

View All Topics
News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02

questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29

questions

2024-03-19: questions

Questions Uploaded on 2024-03-19

Dismissible in 10 seconds