Ufahamu questions | form four Kiswahili

(2601) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Mtu hutembea njiani akajikwaa, ukucha ukang’oka au pengine hata kubwagwa chini vibaya na kisiki, kisha mtu huyu hugeuka na akakiangalia kisiki hicho, ambacho pengine huwa hata hakitazamiki.
Kama kisiki kimkwazavyo mtu atembeaye, pia mikasa mbalimbali, midogo kwa mikubwa,
huwakwaza na pengine hata kuwabwaga chini binadamu katika maisha yao. Jinsi baadhi ya mikasa hii ilivyo adhimu, mtu anapokumbuka huweza kulia. Kwa upande mwingine mtu hujionea fahari alivyopambana na mikasa hiyo kwa ujasiri hadi akaishinda au kuikwepa. Tukio kama hili hufanya shajara la mambo bora ya kukumbukwa maishani.
Maisha ya shule ni mazuri, lakini mara nyingi huwa magumu na hasa lile wingu jeusi la mitihani likaribiapo. Wanafunzi hupuuza sheria kama vile kwenda madarasani, michezoni na pengine hata kula, wakajibanza mahali pa faragha wakajisomea. Nyakati zipendwazo ni usiku wa manane, kwa kujua kuwa kila mtu amelala na kuwa hayupo mwalimu wa zamu awezayo kuzuru shule wakati huo.
Wanafunzi wenye bahati hunufaika sana kwa mpango huo wala hawagunduliwi. Wengine mara hugunduliwa wakapewa adhabu ambayo huridhika kuifanya kwani n zi kufa kwenye kidonda si hasara .
Siku hiyo ilikuwa Jumapili, nami nikajiunga katika ngoma ya kusoma na wenzangu wanne, wawili wao walikuwa viranja wa madarasa. Ilipata saa nane za usiku nasi tukaingia katika chumba cha kuoneshea picha, tukafunga mlango kwa funguo na komeo. Baada ya kuhakikisha kuwa hapana hata mwonzi mdogo wa taa uliotambaa nje, tulitoa ala zetu, kila mtu akashughulika na hamsini zake.
Hapakupita saa moja, mara tunasikia mlango unabishwa hodi, “fungua mlango! tokeni sasa hivi.” Sauti hiyo ilikuwa ya mmoja wa wanafunzi wa shule yetu. Mwanafunzi huyu aliandamana na mtu ambaye tulimtambua kwa sauti kuwa alikuwa Tatu, dada mkuu wa shule. Mioyo ilianza kutudunda kwa hofu, damu zetu zikawa karibu kuganda. Mara nilipata fahamu nikazima taa, lakini kwa bahati mbaya chumba hicho hakikuwa na madirisha ambayo kwayo tungeliweza kutoka. Kumbe mwanafunzi huyo naye alipata maarifa, alipanga viti kimoja juu ya kingine, akapanda juu na kuchungulia ndani katika mwanya uliokuwa karibu na dari. Kumulika ndani akamtambua Dora.
Dora! Dora! fungueni mlango na tokeni sasa hivi!” akang’aka, lakini tukapiga kimya humo ndani.
Mwanafunzi huyo alipoona ameshindwa kututoa, alifanya hila ya kumwita mwalimu mkuu. Naam, sauti ya simba huweza kumdondosha chini panya aliyejificha darini. “Dora fungua mlango sasa hivi!” alinguruma, sote tulibaki tumeduwaa. Dora akafungua mlango, “u shikwapo shikamana” wahenga walisema, mlango ulipofunguliwa mimi nilibana nyuma yake bila mtu kufahamu. Mwalimu mkuu aliwasha taa akachungulia ndani. Kuona hakuna mtu alizima taa akaondoka zake kwenda kuwadadisi wenzangu. Moyo ulishuka pwaa! nikatoka huku nagwaya mwili mzima, nikakimbia kwa mashaka makubwa hadi benini kwangu. Kwa vyovyote vile nilijua nilikuwa ndani.Hazikupita hata datika tano tokea nijitupe kitandani nikashtukia taa zinawashwa mabwenini. Kumbe mwalimu mkuu, mwalimu wa zamu na Tatu, wakisaidiana na akina dada kadhaa walikata shari wafanye uchunguzi wa shule nzima, ili kuona iwapo wanafunzi wote walikuwepo. Ama kweli “s iku za mwizi arobaini,” wanafunzi wapatao kumi na watano walikuwa mjini ambako kulipigwa muziki
na bendi mashuhuri kutoka Dar es Salaam. Asubuhi niliamka kichwa kizito nikauhisi mwili sio wangu. Masomo kuanza tu likapitishwa tangazo likiwaita wale wenzangu niliokuwa nao usiku na wale waliotoroka. Ilipofika saa nne, tukakuta wote wanafunga virago, nikaanza kuwa na matumaini kuwa ama kweli niliponea chupuchupu.

Maswali
(a) Fafanua maana za misemo ifuatayo kama ilivyotumika katika habari uliyosoma:
(i) Nzi kufa kwenye kidonda si hasara.
(ii) Kila mtu akashughulika na hamsini zake.
(iii) Ushikwapo shikamana.
(iv) Siku za mwizi arobaini.
(b) Unafikiri kwanini uongozi wa shule aliyokuwa anasoma mwandishi ilipiga vita tabia ya
wanafunzi kusoma wakati wa usiku wa manane.
(c) Una mawazo gani kuhusu kitendo cha Tatu kufuatilia mienendo ya wanafunzi wenzake hasa kwa usiku ule wa manane.
(d) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano (5).

Answer / Solution

UNSOLVED

(2602) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Baba alikuwa na wajibu maalum wa kuhakikisha usalama wa familia yake. Ilimbidi awe na nyumba watakamoishi mke na watoto. Nyumba zilijengwa kwa mitindo tofauti katika sehemu mbalimbali hapa nchini. Wanyakyusa walikuwa na ujenzi wao ambao ni tofauti na ule wa Wahaya. Wote wakijenga kwa ufundi wa kuvutia sana. Serikali yetu imehifadhi kwa njia ya makumbusho nyumba zilizojengwa na wakazi wa sehemu mbalimbali hapa nchini wakitumia mitindo yao ya asili. Nyumba hizi zipo katika kijiji cha makumbusho kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Baba akishirikiana na mama walikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa jamii yao ilipata chakula cha kutosha. Mapema watoto nao walishiriki katika shughuli za kutafuta na kuandaa chakula.
Jamii nyingine hapa nchini zilikuwa zikishughulika na ufugaji tu. Maisha na utajiri wa jamii hizi ulitegemea wanyama. Tangu utoto wao, mafunzo makuu yalihusu ufugaji. Kwa mfano, mtoto wa kimasai alijifunza kuchunga na kulinda wanyama wake tangu utotoni. Ilimbidi awe askari hodari, aweze kupambana na maadui waliotaka kuteka wanyama wao. Alitakiwa aweze kupigana na wanyama wakali porini wenye kuishambulia mifugo. Kumuua simba ilikuwa ni ishara kubwa ya uhodari wa kijana wa kimasai. Mafunzo ya kumwandaa kijana huyo, tangu utoto wake kwa kazi zitakazomkabili katika maisha, yalichukua sehemu kubwa ya malezi.
Kijana wa Kihaya alikabiliwa na mazingira tofauti sana na yale mwenzie wa kimasai. Wahaya ni wakulima, ufugaji ulichukua sehemu ndogo tu katika shughuli zao za kiuchumi. Wahaya hulima mazao ya kudumu kama vile migomba, mashamba yao yalihitaji ulinzi na utunzaji mzuri. Hivyo serikali imara yenye kuhakikisha amani katika nchi ili raia waweze kuendelea na kazi za kilimo kwa amani, ilihitajika. Pia Wahaya walihitaji nyumba za kudumu; maana hali ya maisha yao haikuruhusu uhamaji wa mara kwa mara kama vile Wamasai. Kwa hiyo mafunzo kamili yalihitajika ili kuwaandaa watoto kwa maisha ya namna hiyo.
Maisha katika sehemu mbalimbali katika nchi yalilazimu ziwepo njia maalum za kuwalea,
kuwafundisha na kuwaandaa kwa yale yatakayowakabili katika siku za usoni.

Maswali
(a) Eleza faida mbili zinazoweza kupatikana kwa kuhifadhi mitindo ya nyumba za asili katika kijiji cha makumbusho.
(b) Unafikiri ni sababu gani iliifanya jamii ya Kimasai kuhamahama?
(c) Kwa mujibu wa habari uliyoisoma vijana walikuwa na jukumu gani katika jamii zao?
(d) Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano kinachofaa kwa habari uliyoisoma.
(e) Andika methali ya Kiswahili inayoendana na aya ya mwisho ya habari uliyoisoma.

Answer / Solution

UNSOLVED

(2603) Question Category: Ufahamu

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Baba alikuwa na wajibu maalum wa kuhakikisha usalama wa familia yake. Ilimbidi awe na nyumba watakamoishi mke na watoto. Nyumba zilijengwa kwa mitindo tofauti katika sehemu mbalimbali hapa nchini. Wanyakyusa walikuwa na ujenzi wao ambao ni tofauti na ule wa Wahaya. Wote wakijenga kwa ufundi wa kuvutia sana. Serikali yetu imehifadhi kwa njia ya makumbusho nyumba zilizojengwa na wakazi wa sehemu mbalimbali hapa nchini wakitumia mitindo yao ya asili. Nyumba hizi zipo katika kijiji cha makumbusho kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Baba akishirikiana na mama walikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa jamii yao ilipata chakula cha kutosha. Mapema watoto nao walishiriki katika shughuli za kutafuta na kuandaa chakula.
Jamii nyingine hapa nchini zilikuwa zikishughulika na ufugaji tu. Maisha na utajiri wa jamii hizi ulitegemea wanyama. Tangu utoto wao, mafunzo makuu yalihusu ufugaji. Kwa mfano, mtoto wa kimasai alijifunza kuchunga na kulinda wanyama wake tangu utotoni. Ilimbidi awe askari hodari, aweze kupambana na maadui waliotaka kuteka wanyama wao. Alitakiwa aweze kupigana na wanyama wakali porini wenye kuishambulia mifugo. Kumuua simba ilikuwa ni ishara kubwa ya uhodari wa kijana wa kimasai. Mafunzo ya kumwandaa kijana huyo, tangu utoto wake kwa kazi zitakazomkabili katika maisha, yalichukua sehemu kubwa ya malezi.
Kijana wa Kihaya alikabiliwa na mazingira tofauti sana na yale mwenzie wa kimasai. Wahaya ni wakulima, ufugaji ulichukua sehemu ndogo tu katika shughuli zao za kiuchumi. Wahaya hulima mazao ya kudumu kama vile migomba, mashamba yao yalihitaji ulinzi na utunzaji mzuri. Hivyo serikali imara yenye kuhakikisha amani katika nchi ili raia waweze kuendelea na kazi za kilimo kwa amani, ilihitajika. Pia Wahaya walihitaji nyumba za kudumu; maana hali ya maisha yao haikuruhusu uhamaji wa mara kwa mara kama vile Wamasai. Kwa hiyo mafunzo kamili yalihitajika ili kuwaandaa watoto kwa maisha ya namna hiyo.
Maisha katika sehemu mbalimbali katika nchi yalilazimu ziwepo njia maalum za kuwalea,
kuwafundisha na kuwaandaa kwa yale yatakayowakabili katika siku za usoni.

Swali:

Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyozidi mia moja (100).

Answer / Solution

UNSOLVED

(2604) Question Category: Ufahamu

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Karibu masikio ya watu wa mahali pengi yalijaa habari za Karama na mashtaka yake. Umaarufu wake wa ghafla ulizungumzwa karibu na mbali. Mtu yeyote wa desturi anapozuka katika umaarufu, huyavuta masikio na macho ya watu wengi kwa sababu jambo kama hili hutokea nadra sana kwa watu ambao bahati mbaya imeshughulika kuwaweka nyuma. Kwa hiyo, siku ya tatu ya baraza ilihudhuriwa na mfalme, watu wenye vyeo mbalimbali, pamoja na nusu moja ya umati mkubwa wa Kusadikika. Fikra zilizochanganyika ziliushika umati huu. Baadhi ya watu walimwajabia Karama
wakamhesabu kama mtu bora wa karne yao. Hawa walitumaini ataokoka lakini wengine waliwaza kuwa Karama alikuwa kama mjinga aliyekuwa akicheza na hatari kubwa iliyofunua taya mbele yake.
Waliokuwa wakimtazamia kuokoka walikuwa na wasiwasi wao; na wale waliokuwa wakimtazamia kuanguka walikuwa na fadhaa yao. Walakini hapana mtu hata mmoja aliyepata kulisema wazo lake.
Bila ya kujua alivyoajabiwa Karama aliendelea kusema mbele ya baraza, “Watu wanaoteswa ndio wanaoyajua mateso yao.” Kusadikika i likuwa c hini ya mateso makubwa sana. Maisha yao yalizungukwa na maradhi na mauti, uadui usiokwisha, nchi iliyokaribia kugeuka jangwa na mwamba na m adhila mengine mazito yaliyowakabili watu. Wanakusadikika walitaka faraja katika mateso haya. Kila jitihada ilijaribiwa ili kuirekebisha saa ya maendeleo ya nchi, lakini mara kwa mara majira yake yalirudishwa nyuma. Kama hili lilifanywa kwa makosa ama kwa makusudi ni siri iliyo ng’ambo ya fahamu zangu hata sasa. Lakini kama siri njema hufichika, ile iliyo mbaya haifichiki hata kidogo. Uchaguzi wa wajumbe ulikuwako lakini hathibitisho ya matokeo ya ujumbe hayakupatikana.
Kusadikika iliishi kuona mjumbe baada ya mjumbe kuadhiriwa n a kuadhibiwa vibaya. Kama washauri hawakudhuriwa na hili lakini watu wengine walidhuriwa sana. Kazi njema za wajumbe wawili zilipotea bure. Manung’uniko ya lawama hii yalikuwa katika hewa yote ya Kusadikika.
Hili lilipotokea serikali iliombwa i ma faima kufanya ujumbe mwingine. Basi mjumbe wa tatu alitakikana ajitolee mwenyewe kwa ujumbe wa Kusini. Wito wa mjumbe wa tatu uliitikiwa na Kabuli; mtu mwenye busara, haya na mcheshi. Yeye alipatikana upesi kabisa kuliko ilivyokuwa kwa mara ya pili na ya kwanza. Misiba ya Buruhani na Fadhili ilikuwa mikubwa ya kutosha kuikongoa mioyo ya bidii katika bawaba zake. Kabuli aliyajua haya yote lakini alikuwa mtu wa moyo wa namna nyingine kabisa. Alikuwa na bidii kubwa kama ile ya siafu athubutiye kukivuka kijito kwa daraja iliyofanywa kwa maiti ya siafu wengine walioelea majini huko na huko. Maji yalijulikana kuwa na asili ya rutuba, mvuke na umeme. Nguvu nyingine za namna mbalimbali zipo pia katika maji. Kama siafu mdudu mdogo na kipofu wakati mwingine haogopi kuzikabili nguvu hizo pamoja na hatari zake kwa sababu njema, basi ni dhahiri kuwa viongozi wa wanadamu wanapoteswa bure bidii za wafuasi wao hutanuka ajabu.
Hapana tishio liwezalo kuukomesha mwendo huu. Kwa hakika utafululiza kuwako duniani mpaka mateso yakome kabisa, na labda wakati huo dunia hii itakuwa njema kama itamaniwavyo kuwa.

Buruhani na Fadhili walitoa sadaka zao bora ili kuyahimiza majilio ya wakati uliotakikana sana. Kabuli aliwaona watu wawili hawa kama wafadhili wakubwa wa ulimwengu. Alitaka kuwa mshirika wao kwa thamani yoyote ya maisha yake.
Kama ilijulikanavyo, Kusini na upande wa dunia yatokako matufani makubwa na baridi kali sana. Kabuli aliyakabili mashaka haya bila ya k igeugeu. Naam, alikuwa kama mtu aliyekuwa akinywa uchungu bila ya kigegezi . Mara mbili alikamatwa akafanywa mahabusu.

Maswali
(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari:
(i) Fadhaa
(ii) Madhila
(iii) Kuadhiriwa
(iv) Ima faima
(v) Kigeugeu
(vi) Kigegezi.
(b) Eleza mchanganyiko wa fikira walizonazo wana wa Kusadikika kuhusu Karama.
(c) Kwanini bidii ya mjumbe wa Kusini imelinganishwa na bidii ya siafu? Toa sababu mbili.
(d) Ujumbe wa mwandishi wa kifungu hiki unahusu nini?

Answer / Solution

UNSOLVED

(2605) Question Category: Ufahamu

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Karibu masikio ya watu wa mahali pengi yalijaa habari za Karama na mashtaka yake. Umaarufu wake wa ghafla ulizungumzwa karibu na mbali. Mtu yeyote wa desturi anapozuka katika umaarufu, huyavuta masikio na macho ya watu wengi kwa sababu jambo kama hili hutokea nadra sana kwa watu ambao bahati mbaya imeshughulika kuwaweka nyuma. Kwa hiyo, siku ya tatu ya baraza ilihudhuriwa na mfalme, watu wenye vyeo mbalimbali, pamoja na nusu moja ya umati mkubwa wa Kusadikika. Fikra zilizochanganyika ziliushika umati huu. Baadhi ya watu walimwajabia Karama
wakamhesabu kama mtu bora wa karne yao. Hawa walitumaini ataokoka lakini wengine waliwaza kuwa Karama alikuwa kama mjinga aliyekuwa akicheza na hatari kubwa iliyofunua taya mbele yake.
Waliokuwa wakimtazamia kuokoka walikuwa na wasiwasi wao; na wale waliokuwa wakimtazamia kuanguka walikuwa na fadhaa yao. Walakini hapana mtu hata mmoja aliyepata kulisema wazo lake.
Bila ya kujua alivyoajabiwa Karama aliendelea kusema mbele ya baraza, “Watu wanaoteswa ndio wanaoyajua mateso yao.” Kusadikika i likuwa c hini ya mateso makubwa sana. Maisha yao yalizungukwa na maradhi na mauti, uadui usiokwisha, nchi iliyokaribia kugeuka jangwa na mwamba na m adhila mengine mazito yaliyowakabili watu. Wanakusadikika walitaka faraja katika mateso haya. Kila jitihada ilijaribiwa ili kuirekebisha saa ya maendeleo ya nchi, lakini mara kwa mara majira yake yalirudishwa nyuma. Kama hili lilifanywa kwa makosa ama kwa makusudi ni siri iliyo ng’ambo ya fahamu zangu hata sasa. Lakini kama siri njema hufichika, ile iliyo mbaya haifichiki hata kidogo. Uchaguzi wa wajumbe ulikuwako lakini hathibitisho ya matokeo ya ujumbe hayakupatikana.
Kusadikika iliishi kuona mjumbe baada ya mjumbe kuadhiriwa n a kuadhibiwa vibaya. Kama washauri hawakudhuriwa na hili lakini watu wengine walidhuriwa sana. Kazi njema za wajumbe wawili zilipotea bure. Manung’uniko ya lawama hii yalikuwa katika hewa yote ya Kusadikika.
Hili lilipotokea serikali iliombwa i ma faima kufanya ujumbe mwingine. Basi mjumbe wa tatu alitakikana ajitolee mwenyewe kwa ujumbe wa Kusini. Wito wa mjumbe wa tatu uliitikiwa na Kabuli; mtu mwenye busara, haya na mcheshi. Yeye alipatikana upesi kabisa kuliko ilivyokuwa kwa mara ya pili na ya kwanza. Misiba ya Buruhani na Fadhili ilikuwa mikubwa ya kutosha kuikongoa mioyo ya bidii katika bawaba zake. Kabuli aliyajua haya yote lakini alikuwa mtu wa moyo wa namna nyingine kabisa. Alikuwa na bidii kubwa kama ile ya siafu athubutiye kukivuka kijito kwa daraja iliyofanywa kwa maiti ya siafu wengine walioelea majini huko na huko. Maji yalijulikana kuwa na asili ya rutuba, mvuke na umeme. Nguvu nyingine za namna mbalimbali zipo pia katika maji. Kama siafu mdudu mdogo na kipofu wakati mwingine haogopi kuzikabili nguvu hizo pamoja na hatari zake kwa sababu njema, basi ni dhahiri kuwa viongozi wa wanadamu wanapoteswa bure bidii za wafuasi wao hutanuka ajabu.
Hapana tishio liwezalo kuukomesha mwendo huu. Kwa hakika utafululiza kuwako duniani mpaka mateso yakome kabisa, na labda wakati huo dunia hii itakuwa njema kama itamaniwavyo kuwa.

Buruhani na Fadhili walitoa sadaka zao bora ili kuyahimiza majilio ya wakati uliotakikana sana. Kabuli aliwaona watu wawili hawa kama wafadhili wakubwa wa ulimwengu. Alitaka kuwa mshirika wao kwa thamani yoyote ya maisha yake.
Kama ilijulikanavyo, Kusini na upande wa dunia yatokako matufani makubwa na baridi kali sana. Kabuli aliyakabili mashaka haya bila ya k igeugeu. Naam, alikuwa kama mtu aliyekuwa akinywa uchungu bila ya kigegezi . Mara mbili alikamatwa akafanywa mahabusu.

Swali:

Fupisha habari uliyosoma hapo juu kwa maneno yasiyopungua mia moja na hamsini
(150) na yasiozidi mia mbili (200).

Answer / Solution

UNSOLVED

View All Topics
News & Updates | Recently
Recent Updates
questions

2024-05-02: questions

Questions Uploaded on 2024-05-02

questions

2024-03-29: questions

Questions Uploaded on 2024-03-29

questions

2024-03-19: questions

Questions Uploaded on 2024-03-19

Dismissible in 10 seconds